Thursday, May 23, 2013

MAJAMBAZI YAVAMIA GARI NA KUPORA FEDHA JIJINI DAR

Matundu matatu ya risasi katika kioo cha gari lililovamiwa na majambazi.


Wanausalama barabarani wakichukua taarifa eneo la tukio.


Majambazi yaliyokuwa na silaha aina ya SMG yakiwa na pikipiki aina ya Bajaj Boxer yamevamia gari ndogo aina ya Toyota Vitz yenye namba za usajili T 929 CCX na kuwajeruhi watu wawili wenye asili ya Asia waliokuwa ndani yake na kuwapora furushi la fedha ambazo mpaka sasa bado haijafahamika ni kiasi gani. Tukio hilo limetokea eneo la Sayansi-Kijitonyama jijini Dar es Salaam.


(PICHA: RICHARD BUKOS NA MUSA MATEJA/GPL)

No comments: