Friday, May 3, 2013

MIAKA ILE 1992 NA HOFU YA UPINZANI KULETA FUJO

Aliyekuwa katibu mkuu wa chama tawla cha TANU enzi hizo Bw. Oscar Kambona akirejea nchini mwaka 1992 akiwa na binti yake, Neema, baada ya kuishi uhamishoni jijini London, Uingereza, kwa takriban miaka 25 kutokana na vuguvugu la kisiasa la wakati huo. 

Picha hii, aliyopiga Ankal uwanjani hapo, haikuwa rahisi kuipata. Wanahabari, waliofika hapo saa kumi alfajiri, walizuiwa kuingia ndani kwa ile hofu kwamba Bw Kambona angetiwa mbaroni na kutokea vuruguru. Ankal alipenya na kuwa wa kwanza kuipata taswira hii ambayo hadi sasa ndiyo iliyobaki kuonesha tukio hilo la kihistoria. Bw Kambona hakukamatwa na hakuna vurugu zilizotokea...

No comments: