Friday, May 10, 2013


Na Joseph Shaluwa
STAA wa filamu za Kibongo, Vincent Kigosi ‘Ray’ amelipuka na kudai kuwa wasanii wa filamu wa Tanzania wanakandamizwa sana na wasambazaji.
Akizungumza na Ijumaa hivi karibuni katika mahojiano maalum, Ray alisema: “Kama nitakuwa sijajifunza kitu kutokana na msiba wa Kanumba (Steven) nitakuwa mjinga. Kama utakumbuka, kwenye mazishi yake  serikali nzima ilikuwa pale, umati mkubwa wa watu ulifurika, kwa nini? Kwa sababu ya thamani yake.
“Msambazaji aliye ‘serious’ ni mmoja kwa sasa na yeye ndiye anayeamua cha kufanya na kwa sababu wasanii tupo wengi, hatuna jinsi. Ukiingia naye mkataba unakuwa umeuza haki ya maisha yako yote. Anakuwa na uhuru wa kupeleka DSTV, Zuku na Channel nyingine zozote bila kukulipa chochote.
“Lakini mimi siwezi kutupa lawama kwa serikali maana tumeshaongea sana. Nawaomba wadau wajitokeze wawekeze kwenye tasnia yetu maana inapanuka na ina soko kubwa ila msambazaji yupo mmoja tu ndiyo maana tunanyonywa.”

No comments: