Monday, April 28, 2014

UCC ARUSHA-MUUNGANO RALLY

Baadhi ya wafanyakazi wa UDSM Computing Centre tawi la Arusha wakiwa nje ya ofisi yao iliyopo jengo la Summit Centre Sokoine road, tayari kabisa kuelekea ofisi ya mkuu wa mkoa kuanza maandamano ya sherehe za miaka 50 ya Tanzania (yaani Muungano). Kutoka kushoto ni Emmanuel Luhwavi, Antidius Gerazi, Stephen Mishita, Rhoda Meena, David Bashosho, Eunice Nkomola na Florence Masebo.

Hivi ndivyo ilivyokuwa wakati wa maandamano hayo. Nyuma ya bango kutoka kushoto ni David Bashosho, Juma Hanzuruni, Stephen Mishita, Florence Masebo, Francisca Kavishe, Eunice Nkomola, Emmanuel Samwel, Rhoda Meena (aliyeinama kidogo) na Hellen Vincent. Huyo aliyenyanyua mikono (nguo ya kijani) na mwenye kilemba kulia ni miongoni mwa wana maandamano sio UCC staff.

Muonekano wa ubavuni wa waandamaji wetu wa UCC-Arusha. Huyo aliyeshika kitambaa mbele ya Florence Masebo ni Margareth Kimaryo

Hii imeonekana vizuri zaidi, kuanzia kulia ni Antidius Gerazi, Hellen Vincent, Juma Hanzuri, Rhoda Meena, Stephen Mishita, Emmanuel Luhwavi, na David Bashosho. Hii ni "Marketting" ya UKWELI.

Waangalie Antidius Gerazi, Rhoda Meena na Stephen Mishita, wanavyoimba kwa furaha WIMBO WA MUUNGANO. Tanzania at 50.

Hapa wakikatiza mitaa ya jiji la Arusha

Kushoto kabisa ni askari aliyehakikisha wana UCC wapo salama kwenye maandamano, anayefuatia ni Margareth Kimaryo, Emmanuel Luhwavi, Eunice Nkomola, Francisca Kavishe, David Bashosho (kwa nyuma) Stephen Mishita na Emmanuel Samwel

Maandamano yanaendelea kuelekea uwanja wa mpira wa miguu SHEIKH AMRI ABIED KALUTA.

Hapa sasa wapo katikati ya stendi kuu ya mabasi na uwanja ambapo ndio hitimisho la maandamano. Wakikata kona kulia mara mbili wanakua weshaingia uwanjani. Kwanyuma yao kushoto ni jengo maarufu la kitega uchumi lijulikanalo kama NAMVUA PLAZA. Taa za barabarani zilizopo kulia kwao (hazionekani pichani) zililazimika kuwaacha wapite hawa waheshimiwa kwanza. Umemuona Meneja Florence Masebo kushoto kabisa alivyojaa tabasamu? ilikua raha kwa kweli.


Hapa ni jukwaa kuu ndani ya uwanja wa SHEIKH AMRI ABEID KALUTA

Vikundi vya burudani havikukosekana, hii ni ngoma ya Kimaasai na nyuma yao ni ngoma ya Msanja kutoka mkoa wa Tanga. Muungano kwanza!!!
==================================================================================
Shukrani za dhati zimwendee Mkurugenzi Mtendaji wa UDSM Computing Centre Mheshimiwa Dr. Ulingeta O.L. Mbamba kwa kutupa nafasi ya kushiriki tukio hili la KITAIFA.

~~~Professionalism, Customer Care and Technological Foresight~~~


NB: Blogger wetu Daudi Mlaule hakuwepo kwenye hafla hii kwa dharura ya kifamilia. Ila waliokuwepo waliwakilisha UCC iipasavyo.

No comments: