Wednesday, May 14, 2014

Stori: Musa Mateja
RAIS wa Wasafi Bongo, Nasibu Abdul  ‘Diamond’ yuko ndani ya bifu zito na mwanamuziki kiwango cha juu kutoka nchini Kenya, Jackson Ngechu Makini ‘Prezzo’ chanzo kikidaiwa ni Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu.

Diva wa filamu za Kibongo, Wema Sepetu 'Beautiful Onyinye'.
Bifu la wawili hao limekuja kufuatia madai kwamba, Prezzo amemtundika Diamond kwenye mtandao akimkejeli kwa kitendo chake cha kurudiana na Wema na kuweka mambo hadharani.
Ilidaiwa kuwa katika maneno yake, Prezzo alikandia akisema anamshangaa Diamond anatamba kuwa ana mpenzi supastaa ambaye ni Wema wakati yeye mwenyewe alishaanguka naye.

Madai yanazidi kusema kuwa Prezzo akaongeza kwa kuandika kwamba, Bongo hakuna mademu masupastaa kwani hata Jokate (Mwegelo) aliyewahi kutamba naye si lolote kwake.
Msanii huyo anadaiwa alikwenda mbele zaidi kwa kusema kama ni ustaa anao yeye mwenye pesa zake na si Diamond ambaye hamfikii kwa lolote.

MASHABIKI WA DIAMOND WAJA JUU
Baada ya kuanika maneno hayo yaliyoonekana kujaa kejeli, mashabiki wa Diamond walimshukia Prezzo na kuanza kumnanga kwa kila mtu anavyoweza mwenyewe ndipo akaanza kuhaha kutaka suluhu kwa Diamond akimuomba meneja wake awakutanishe.

Mkali wa Bongo Fleva nchini, Nasibu Abdul 'Diamond'.
DIAMOND NAYE AWA MBOGO
Akizungumza kwa hasira na paparazi wetu usiku wa kuamkia Mei 11, mwaka huu ndani ya Ukumbi wa Element uliopo Masaki jijini Dar es Salaam, Diamond alisema kufuatia matusi hayo hatarajii kufika kwenye vikao vya usuluhishi na mtu yeyote yule.

“Nimekasirishwa sana na huyu jamaa (Prezzo) amenitukana kwenye mtandao mimi na demu wangu (Wema) huku akijua sijawahi hata siku moja kujihusisha na yeye kwa jambo lolote lile, daa!” alihamaki Diamond.
HASIRA ZOTE HIZO ZIMETOKA WAPI?
Diamond aliyasema hayo baada ya meneja wa Prezzo aliyejulikana kwa jina moja la Asa kumtaka Mbongo Fleva huyo wakutane yeye akiwa na Prezzo ili wamalize tofauti zao.

“Meneja wake aliniita eti tukakae kikao kuyaongea, mimi sioni sababu ya kukutana na Prezzo, yeye ndiye alianza kunitukana hivyo kama anataka kweli kuelewana na mimi basi arejee tena mtandaoni akaombe radhi, nitamuona muungwana.
“Unajua katika muziki ni wachache sana wenye uwezo wa kutumia ustaarabu katika maamuzi yao, wengi wanaamini kumtusi mtu ndiyo njia pekee ya kupandisha jina au kumfanya abusti ngoma yake kumbe huwa ni njia mojawapo ya kujishushia heshima hasa kwa watu wenye busara walio nyuma yake.”
Mkali wa muziki kutoka Kenya, CMB Prezzo.
ANACHOKIAMINI DIAMOND
Akiendelea kuzungumzia ishu hiyo, Diamond alisema anachoamini yeye, Prezzo alifanya vile ili apate kiki kupitia mgongo wake.

“Najua kama alifanya hayo kwa kufurahisha nafsi yake basi ilisuuzika. Anachotakiwa kukifanya kwa sasa ni kurudi mtandaoni akaandike mazuri yangu.
“Kwanza mimi sina hata chembe moja ya chuki na yeye ingawa amenioneshea uswahili wa hali ya juu,” alisema Diamond.

WAKUTANA, WAFUNGIANA VIOO
Hivi karibuni, wawili hao walikutana katika Ukumbi wa Element, Masaki, Dar ambapo Prezzo alikuwa akifanya shoo lakini walifungiana vioo.

TURUDI NYUMA
Siku za nyuma, iliwahi kuripotiwa na vyombo mbalimbali vya habari vya Tanzania na Kenya (hasa magazeti) kuhusu kuwepo kwa uhusiano wa kimapenzi kati ya Wema na Prezzo ambao ulidumu kwa muda mfupi baada ya Wema kumwagana na Diamond.

No comments: