Wednesday, April 1, 2015

HABARI MBALI MBALI ZA LEO-KWA HISANI YA GPL

KIMENUKA BUNGENI; WABUNGE WAPIGA KELELE WAKITAKA MAJIBU KURA YA MAONI

Mbunge wa Ubungo (Chadema) akichangia mada bungeni.
SPIKA wa Bunge, Anne Makinda ameamua kulihairisha bunge hadi hapo baadaye baada ya vurugu kuibuka kwa baadhi ya wabunge wakitaka hoja ya kuhairisha mchakato wa kura ya maoni ijadiliwe na kura ya maoni isogezwe mbele maana muda hautoshi.
Mbunge wa Ubungo (Chadema), John Mnyika alisimama na kusema: "Nimesimama kupata idhini kwa mujibu wa kanuni ili shughuli za bunge zisitishwe badala yake tujadili zoezi la uandikishaji nchi nzima mpaka sasa zoezi halijakamilika hata kwa mkoa mmoja tu wa Njombe, jambo hili ni la dharura na ilishatolewa na ukaagiza kamati ishughulikie, majibu tupate kikao hiki na leo tunafunga mkutano hamna kitu"

Spika Makinda alijibu: Hoja hii inafanana na ile ya kwanza, nimesema majibu mtajibiwa baadae ndipo wabunge waliposimama na kupiga kelele wakitaka majibu na Spika Anne Makinda akalazimika kusitisha bunge hilo kwa muda.
===========================================================


MWANDISHI WA UJERUMANI ALIFAGILIA GAZETI LA ‘UWAZI’

Meneja Mkuu wa Global Publishers, Abdalah Mrisho (kushoto), akiongea na mwandishi Hawa Bihoga wa Idhaa ya Kiswahili Ujerumani (DW) ofisini kwake Sinza-Bamaga jijini Dar es Salaam. Bihoga alifika hapo kulipongeza gazeti la Uwazi  na mwandishi Haruni Sanchawa. Mrisho akiagana  na Bihoga.
MWANDISHI  wa Shirika la Habari Idhaa ya Kiswahili Ujerumani (DW),  Hawa Bihoga,  ametoa pongezi kubwa kwa kampuni ya Global inayochapisha magazeti ya Championi , Ijumaa,  Amani,  Ijumaa Wikienda , Risasi na Uwazi kwa kuibua matukio ya kipeke yanayosikitisha jamii kama lile lililoandikwa  kuhusu watoto watatu wakubwa wagonjwa wa akili waliofungiwa ndani na mama yao kwa miaka kumi.

Bihoga alimpongeza  mwandishi na Global Publishers, Haruni Sanchawa, kwa kufika katika eneo hilo na kufanikisha habari hiyo kufika gazetini.  Aliongeza kwamba juhudi hizo ziliiwezesha serikali kujionea  hali halisi  ambayo  baadhi ya jamii huishi katika mazingira magumu.
Mwandishi huyo wa Ujerumani pamoja na kuonana na mwandishi huyo alipokuwa katika ofisi za Global, alifanya pia mazungumzo na Meneja Mkuu wa kampuni,  Abdalah Mrisho, ambapo alimpongeza kwa mipango bora ya kampuni kwa jumla.
Naye Mrisho alisema kampuni ilikuwa imefarijika sana kutokana na kupatikana  kwa habari hiyo akisisitiza kwamba gazeti la Uwazi siku zote limekuwa likibua mambo mazito kama hayo.
Aliahidi kwamba habari nyingine nyingi kama hizo zitaendelea kufuatiliwa kwa gharama yoyote ili kuisaidia jamii ambayo inaishi katika mazingira kama hayo.

 

===========================================================

JENERALI MUHAMMAD BUHARI: RAIS MPYA NIGERIA

Rais mteule wa Nigeria Jenerali Muhammadu Buhari.

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi nchini Nigeria, INEC, Attahiru Jega amemtangaza rasmi Kiongozi wa wa chama cha upinzani cha Nigeria Jenerali Muhammadu Buhari kuwa rais wa taifa hilo kubwa barani Afrika baada ya kumbwaga rais wa zamani Goodluck Jonathan.
Wafuasi wa Jenerali Buhari wakishangilia…

 

===========================================================

 

WAZIRI LUKUVI AHITIMISHA ZIARA YA SIKU MBILI ASHUHUDIA UTENDAJI WA NHC

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Vangimembe Lukuvi akikagua mradi wa nyumba za gharama nafuu za makazi za Kibada, Kigamboni alipokuwa akikagua mradi huo jana mchana.
Nyumba za gharama nafuu za NHC Mwongozo, Kigamboni Dar es Salaam zinavyoonekana wakati Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Vangimembe Lukuvi alipozitembelea.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi…===========================================================

ASKOFU GWAJIMA ATOLEWA POLISI KWA DHAMANA

Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima akiwa kwenye baiskeli ya wagonjwa Hospitali ya TMJ Dar es Salam jana mchana akielekea  Kituo cha Polisi cha Oyterbay kupewa dhamana.
Gwajima akiingia kwenye gari huku akiwa na maumivu makali wakati akielekea kituoni hapo kupewa dhamana.
Wanahabari wakitoka kituo cha polisi Oysterbay kufuatilia …

 

===========================================================

 

TSJ WAPEWA ZAWADI ZA VIFAA VYA HABARI

Mkuu wa Chuo cha Uandishi wa Habari cha TSJ, Blandina Semaganga(kushoto), Sweetbeth Bruno wa The Sanitarium Kliniki (katikati) pamoja na Dr. Fadhil Emily.
Wanachuo wa TSJ wakifurahia msaada huo.
Mwanachuo wa TSJ, Florida Moses akitumbuiza katika hafla hiyo.


No comments: