
KIJANA Mtanzania, Salum Kombo (18) ameuawa kwa kuchomwa kisu nchini Uingereza.
Rafiki wa kijana huyo ndiye aliyemchoma kisu baada ya malumbano waliyofanya kupitia mtandao wa kompyuta kwenye tovuti ya Facebook.
Kijana huyo alikuwa akisoma Sanaa katika chuo cha Tower Hamlets kilichopo London ya Mashariki.
Kombo aliaga dunia baada ya kuchomwa kisu mara kadhaa kifuani na shingoni akiwa karibu na nyumbani kwao.
Imedaiwa kuwa mtu aliyemchoma kisu ni rafiki yake mkubwa na amefanya hivyo baada ya Salum kumtumia taarifa iliyomkera wakati akijibu hoja yake baada ya kukataliwa kuhudhuria hafla iliyoandaliwa na akina Kombo.
Kombo alichomwa kisu hicho Jumapili kiasi cha yadi 400 kutoka makazi ya shangazi yake ambaye ndiye alikuwa akimlea.
Imedaiwa kuwa, kijana mwingine baada ya kukasirishwa na ujumbe huo alimfuata Salum akijifanya hakuna tatizo kati yao na kabla ya kumchoma kisu huku akiwa anamkumbatia.
Kombo aliwasili nchini Uingereza akitokea Tanzania miaka saba iliyopita na alikuwa akiishi na shangazi yake huko Bow, London ya Mashariki.
Majirani wa akina Kombo wamedai kuwa, kabla ya kijana huyo kuchomwa kisu alikuwa akiimba nyimbo za Krismasi na wenzake.
Imeelezwa kuwa hali ya shangazi yake Salum si nzuri baada ya taarifa za kifo cha kijana wake.
Gary Byrne, 46, alisema alikuwa anaona jinsi uhai unavyomtoka kijana huyo taratibu dakika chache kabla ya watu wa huduma ya kwanza kufika na kumsaidia.
Kijana huyo alipoteza maisha dakika 20 tu baada ya kuanza kupewa huduma ya kwanza.
Kijana huyo alipata majeraha makubwa katika kifua na shingoni. Haya ni mauaji ya 13 kutokea kwa vijana katika jiji la London mwaka huu.
Polisi wanamshikilia kijana aliyehusika na mauaji hayo na walikuwa wanatarajia kumfikisha mahakama ya Thames jana
Kwa maelezo ya Kiingereza kopi hii link hapa chini ui paste ktk address bar then gonga enter key.
http://www.thesun.co.uk/sol/homepage/news/2781029/Facebook-insult-led-to-killing-in-the-street.html#ixzz0aP7d8QHr
No comments:
Post a Comment