This blog is for critical thinkers, people with open mind, ready to accept criticisms and work on them. Sharing the know-how, skills and experiences of Life and Technology at large. You are warmly welcome!! ---------------------------------------------------- Blogu hii ni kwa ajili ya wenye fikra makini wapendao kupokea na kufanyia kazi ukosoaji. Walio na mtazamo chanya tena mpana katika kushirikishana maarifa, ujuzi na uzoefu wa maisha na teknolojia kwa ujumla wake. Karibuni sana !!!
Wednesday, July 14, 2010
Maandamano kumtetea Justin Nyari wa Arusha
Umati mkubwa wa wananchi kutoka Vijiji na Vitongoji vya Kata ya Mererani wakifanya Maandamano makubwa ya kupinga kitendo cha mfanyabiashara na mchimbaji maarufu wa madini ya tanzanite, Justine Nyari kutuhumiwa na jeshi la polisi kuhusika na wizi wa madini
mmoja wa wananchi hao akiohojiwa na waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari.
Na Novatus Makunga,
Arusha( Kwa Hisani ya Mchuzi Blog)
Umati wa kutoka Vijiji na Vitongoji vya Kata ya Mererani jana alasiri walifanya Maandamano makubwa wakipinga kitendo cha mfanyabiashara na mchimbaji maarufu wa madini ya tanzanite Justine Nyari kutuhumiwa na jeshi la polisi kuhusika na wizi wa madini
Wananchi hao baadhi wakiwa wanatembea kwa miguu na wengine kwa pikipiki wengi wao wakiwa ni wachimbaji katika migodi ya tanzanite ya Mererani walilizonga gari la Nyari aina ya Toyota Landcruiser mara tu baada ya kuwasili katika mji mdogo wa Mererani
Wananchi hao wakiwa na nyuso za hasira walisema kitendo cha Nyari kutuhumiwa kuhusika na wizi huo ni njama za kutaka kumchafulia kunakofanywa na wapinzani wake wa kibiashara na kisiasa
Wakizungumza na Waandishi wa habari wananchi hao Joyce Munisi,Janeth Cleopa,John Akyoo, Riziki Alfonce Ally Sibuga na Philipo Mungure walidai wafanyabiashara hao wanatumia nguvu ya fedha walizonayo kutaka kumwangamiza Nyari.
Walisisitiza kwamba Kitendo cha Wafanyabiashara hao kumsingizia Nyari kwamba anahusika katika uporaji wa madini ya Tanzanite kutoka Ofisi ya kampuni ya Manga Gems za mini Arusha ni cha hatari sana
Walisema Nyari ni wafanyabiashara mwenye roho ya utu kwani amekuwa akitoa msaada kwa makundi yanayoiswhi kwa ufukara yakiwemo ya wajane, yatima na kwa wazee wasiojiweza katika eneo la Mererani tofauti na wengine wenye uwezo kama wake.
Kutokana na tuhuma za madai hayo mapema wiki iliyopita kamanda wa polisi mkoa wa Arusha Basilio Matei alinukuli na baadhi ya vyombo vya habari ya kwamba jeshi hilo linamsaka Nyari
Hata hivyo Nyari ambaye wakati huo alikuwa mjini Dodoma kwa shughuli za kibiashara alilazimika kurejea mjini Arusha na kwnda kujisalimisha polisi ambao swalimhoji kwa zaidi ya saa mbili
Wananchi hao wameiomba Serikali na Jeshi la Polisi kuwa makini na taarifa zinazofikishwa kwao kwani baadhi ya taarifa hizo zinalenga kuchafuliana katikla jamii
Kwa upande wake Nyari halikata kuzungumza na waandishi wa habari kuhusiana na kitendo cha kuhojiwa na polisi na pia kitendo cha umati wa wananchi kukusanya na kupinga kuhutumiwa kwa wizi huo
“Jamani mimi sina lolote la kuongea sina cha kuongea kwenye magazeti, wala redio ama telvisheni na waomba wananchi pigeni magoti muniombee kwa Mungu ukifika wakati nitaongea,”Alisema Nyari .
Kwa upande wake, Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Arusha Basilio Matei alikanusha kutoa taarifa za kwamba mfanyabiashara huyo anahusika na wizi wa Madini
Kamanda Matei amesema kuwa amreshangazwa kukuta taarifa hizo katika magazti ilihalio yeye hakuzitoa .
Amefafanua kwamba polisi walipokea taarifa kutoka kwa walinzi wa Kampuni iliyoibiwa madini kuwa Nyari ndiye aliyeuziwa madini yaliyoibiwa kutoka katika ofisi ya Manga Gems.
Hata hivyo kwa mujibu wa Matei Polisi walipopata taarifa hizo waliamua kumhoji Nyari na kufanya upekuzi Ofisini kwake na Nyumba lakini hakuna kitu ambacho Polisi walifanikiwa kupata na hivyo wanaendelea na upelelezi
Amevitaka vyombo vya habari kuepuka kupotoisha habari zinazoweza kusababisha mtafaruku ndani ya jamii ili viandike ukweli kuhusu matukio mbalimbali
Tukio lilitokea usiku wa April 14, mwaka madini ya tanzanite na fedha taslimu vyote vikiwa na tham,ani ya zaidi ya shilingi milioni 100 yaliibiwa katika ofisi za Manga Gems ambapo walinzi wawili waliokuwa wanalinda walitoweka.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment