Na Innocent P. M. Mungy
Guadalajara Mexico,
Tanzania imefanikisha kukua kwa sekta ya TEKNOHAMA (Teknolojia ya habari na Mawasiliano (ICT) kutokana na sera yake ya TEKNOHAMA ya mwaka 2003 pamoja na Mfumo wa Leseni wa Muingiliano wa Teknologia (Convergence Licsensing Framework) inayoutekeleza.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia Profesa Peter Msolla alipokuwa anahutubia Mkutano Mkuu wa ITU 2010 (ITU Plenipotentiary unaofanyika hapa Guadalajara Mexico.
Prof. msolla alisema sera hiyo iliyopelekea kuundwa kwa mfumo huo, vimewezesha sekta ya mawasiliano kukua kwa kasi nchini na kuleta maendeleo kwa kipindi kifupi.
Alitaja maeneo yanayoonesha kukua kwa sekta hio kuwa ni pamoja na kuwepo kwa makampuni saba ya simu za mkononi yanayofanya kazi nchini na mengine manne yanayojenga mitandao tayari kuanza kazi.
Hali kadhalika alisema matumizi ya simu za mkononi yamekuwa kutoka watumiaji karibu laki mbili hadi kufikia takkribani milioni 18 hivi sasa.
Watumiaji wa intenet pia wameongezeka kutoka asilimia 0.06 mwaka 1994 hadi asilimia 12 hivi sasa.
Mkutano huo unaendelea jijini Guadalajara na masuala muhimu ya maendeleo ya sekta ya habari na mawasiliano yatajadiliwa na kufikia maamuzi muhimu kwa maendeleo ya baadae.
Mkutano huo ulifunguliwa na Rais wa Mexico Felipe Calderón Hinojosa aliyewataka wajumbe wa mkutano huo kuwa makini katika majadiliano na kufikia maamuzi yatakayoleta maendeleo ya TEKNOHAMA kwa watu wote duniani.
No comments:
Post a Comment