This blog is for critical thinkers, people with open mind, ready to accept criticisms and work on them. Sharing the know-how, skills and experiences of Life and Technology at large. You are warmly welcome!! ---------------------------------------------------- Blogu hii ni kwa ajili ya wenye fikra makini wapendao kupokea na kufanyia kazi ukosoaji. Walio na mtazamo chanya tena mpana katika kushirikishana maarifa, ujuzi na uzoefu wa maisha na teknolojia kwa ujumla wake. Karibuni sana !!!
Friday, March 25, 2011
Imani yako ITAKUPONYA
WAGONJWA kadhaa waliokunywa dawa ya Mchungaji Ambilikile Masapila (pichani), wamemuaibisha babu huyo kwa kudai kuwa hawajapona maradhi yao baada ya kupata kikombe.
Wagonjwa hao waliozungumza na gazeti hili juzikati, walisema ni zaidi ya siku saba sasa baada ya kupata kikombe cha babu lakini hali zao kiafya bado mbaya.
“Nilikunywa dawa ya babu siku kumi zilizopita, sijapata nafuu ya ugonjwa wangu wa kisukari,” alisema Sudi Makwa aliyejitambulisha kuwa ni mkazi wa Mikocheni B jijini Dar es Salaam.
Akisimulia jinsi alivyofanikiwa kunywa dawa ya babu, Makwa alisema alipata lifti ya mzito mmoja (hakumtaja jina) na walipofika Kijiji cha Samunge walipenyezwa na askari, hivyo kufanikuwa kupata dawa.
“Mimi nilipofika Arusha nilikodi pikipiki, ilikuwa rahisi kwangu kumfikia babu kwani tulipenya na nikanywa dawa lakini sijapata nafuu,” alisema Makwa.
Madai kama hayo yalitolewa na wanawake wawili maarufu mjini hapa walioomba majina yao kuhifadhiwa ambao walidai kuwa, walipenya katika foleni kutokana na kujulikana kwao lakini walisisitiza kuwa hawajapona magonjwa yanayowasumbua.
Naye Jerome Mpondwa, mkazi wa Sinza Mori, Dar alisema alikwenda kwa babu zaidi ya siku 15 zilizopita na kunywa dawa lakini bado kisukari kinamsumbua.
Uchunguzi wa gazeti hili umebaini kuwa moja ya sharti la babu ni kukaa katika foleni bila kufanya ujanja wa kuwapita uliowakuta.
Mwandishi wetu ambaye aliwahi kuzungumza na babu hivi karibuni alimkariri akisema kuwa watu wanaokiuka masharti, wanapokunywa dawa yake inakuwa kama vile wamekunywa juisi tu na kamwe hawawezi kupona.
Sharti lingine alilolisema mchungaji huyo ni kwamba hairuhusiwi kurudia dawa au vitendo vilivyosababisha wapate maradhi waliyotibiwa hasa zinaa ambayo inachangia kuenea kwa Ukimwi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment