Kocha Mkuu wa timu ya Taifa,Jan Poulsen akiwa na baadhi ya watoto wa shule katika viwanja vya sheikh Amri Abeid jijini Arusha leo.Na Mwandishi Wetu
Kampeni ya malaria imefanyika jijini Arusha jana katika kiwanja Sheikh Amri Abeid na kuhuduriwa na kocha wa timu ya Taifa ya Tanzania pamoja na mkurugenzi wa Ufundi wa TFF Sunday Kayuni.
Ambapo shule zaidi ya nane zimeshiriki mashindan hayo ikiwa ni katika kuunga mkono juhudi za kuhakikihsha kuwa Malaria haikubaliki miongoni mwa jamii ya Kitanzania.
Shindano hilo limeandaliwa na taasisi ya John Hopkins University ya marekani tawi la tanzania.
Awali akifungua michezo hiyo katibu tawala wa jiji la Arusha, bibi. Emmy Lyimo alisema serikali imefurahishwa sana na juhudi za taasisi hiyo katika kuhakikisha jamii inapiga vita ugonjwa wa malaria na kusema huu ni mchango mkubwa sana uliowahi kupatikana katika juhudi za kupambana na malaria nchini Tanzania.
Alisema kilele cha siku ya malaria ulimwenguni kitafanyika katika jiji la Arusha tarehe 25/04/2011, hivyo kutafunguliwa kliiki ya kusaidia kukumbusha jamii kuhusu umuhimu wa kutumia Vyandarua vyenye dawa ya kuuwa mbu na pia kutumia dawa kwa usahihi pale mtu anapokutwa na wadudu wa malaria.
Aliwataka wanajamii kote nchini kuungana kwa pamoja katika kuupinga ugonjwa huo na pia kuzingatia kauli mbiu ya serikali ya MALARIA HAIKUBALIKI NA TUUNGANE KUITOKOMEZA.
Kwa upande wake mkurugenzi wa ufundi wa TFF Bw. Sunday Kayuni alisema wameamua kufanya michezo hiyo kwa watoto kutokana na ukweli watoto ndio tabaka linaloongoza kwa vifo vya maaria kote ulimwenguni ambapo barani Afrika pekee kila baada ya sekunde thelathini mtoto mmoja hupoteza maisha.
Jumla ya zaidi ya watoto mia tano wameshiriki katika michezo hiyo ambapo licha ya kupata mafunzo lakini wanapatiwa vyeti na vyandarua kwa kila mshiriki kwaajili ya kuwasaidia kwenda kuwa mabalozi wa kudumu wa malaria kote ulimwenguni
No comments:
Post a Comment