Na Mwandishi Wetu
Kwa jicho la juu, warembo mastaa muonekano wao ni bei mbaya a.k.a expensive, wapo wanaovunja benki ili kuwanasa bila kujua siri nzito iliyopo, kumbe asilimia 90 ni bei chee.
Ingawa wapo wenye misimamo yao na wasiozuzuka na ‘usistaduu wa kideoni’, idadi kubwa ya mastaa wanaotibua ‘kitaani’ na kwenye vyombo vya habari ni sababu ya tasnia nzima kuingia doa.
Ijumaa ‘The Udaku Master’, kupitia uchunguzi wake limebaini makundi matatu ambayo warembo hao wameyatengeneza, mosi likiwa la wale wanaojiheshimu (watulivu, wenye msimamo), pili ni la wale bei mbaya ‘expensive’ (kuwapata inabidi ujipinde), tatu lenye memba wengi ni la bei chee.
Ripoti ya Ijumaa pia ina kundi la warembo ambao pamoja na kwamba hawakuwekwa kwenye kundi lolote kati ya hayo matatu lakini tabia na vitendo vyao vimekuwa vikitia ‘kinyaa’ na kusababisha jamii iwashushe hadhi.
WANAOJIHESHIMU
Mastaa ambao mpaka sasa wameonesha msimamo na wanajiheshimu ni Malkia wa Afro Pop Bongo, Judith Wabura ‘Lady Jaydee’, (aliyepakatwa na mumewe pichani) mtangazaji nyota aliye pia mwanamuziki, Fina Mango ‘Ndege Mnana’ na staa wa filamu, Ndumbangwe Misayo ‘Thea’.
Wengine wenye msimamo ambao hawajanaswa na skendo ya aina yoyote mpaka sasa ni mtangazaji Zamaradi Mketema, mrembo aliyetisha kwenye Hip Hop, Zainab Lipangile ‘Zay B’, Miss Tanzania 2007/08, Richa Adhia na Miss Tanzania namba mbili 2006/07, Jokate Mwegelo.
Wapo wengine wanaoonekana wanajiheshimu lakini Ijumaa limewaondoa baada ya kubaini kasoro zao za chini chini, huku baadhi likitaka kujiridhisha zaidi.
BEI MBAYA
Kundi hili, linaundwa na mastaa wenye msimamo kwa wanaume ‘makapuku’ lakini ni wepesi mbele ya wafanyabiashara na wanasiasa wanaojua ‘kukata mpunga’.
Ingawa majina yao yanahifadhiwa kwa sasa, Ijumaa lina orodha ya mastaa 13 ambao wamekuwa wakigawa mapenzi kwa wanaume matajiri kwa matarajio ya kupata malipo makubwa.
Hata hivyo, baadhi yao wamejikuta wakiaibika baada ya kunyang’anywa magari ambayo walihongwa na wanaume kama malipo ya kuwapa mapenzi ya ‘nipe nikupe’.
BEI CHEE
Uchunguzi wa gazeti hili umebaini kwamba, mastaa wengi wanaounda kundi kubwa ni bei chee kwa sababu hutoa penzi ama kwa gharama nafuu au bure ili kutimiza matakwa yao ya kuwa maarufu.
Ijumaa limebaini kwamba, warembo wengi hasa waigizaji, hujirahisi kwa maprodyuza mastaa ili wapate kuonekana kwenye filamu zinazotengenezwa.
Prodyuza mmoja aliliambia gazeti hili hivi karibuni kuwa warembo wengi kabla ya ‘kuuza’ sura kwenye filamu mbalimbali, huwapa ofa ya unyumba baadhi ya maprodyuza.
“Hii ipo wazi kabisa, tasnia inaundwa na watu wengine hatari kabisa. Baadhi yao walikuwa hawajatulia huko mtaani na wengine wameshindwa maisha, kwa hiyo kutoa unyumba kwa prodyuza ili watoke hawaoni kazi.
“Ni wengi sana wanajirahisi. Unaweza kuwaona ni mastaa kwenye filamu lakini nje wanatongoza wanaume ovyo,” alisema prodyuza huyo (jina tunalo).
Ukiachana na prodyuza huyo, hivi karibuni gazeti ndugu na hili, Ijumaa Wikienda liliandika habari ya staa mmoja wa filamu kumpigia simu mbunge wa jimbo moja la Morogoro na kumuomba wawe pamoja.
Mbunge huyo aliliambia Ijumaa Wikienda kuwa, mrembo huyo alikuwa anamheshimu lakini alimshusha thamani baada ya kumtongoza bila aibu.
Aidha, Ijumaa inaifanyia kazi orodha ya mastaa 22 ambao wanatajwa kuwa kimeo kuliko wengine kwa kuwa na tabia ya kutongoza au kujitongozesha kwa wanaume.
KUNDI LINALOCHAFUA TASNIA
Uchunguzi umebaini kuwa, mastaa wanaoongoza kwa skendo, wamekuwa wakichafua hali ya hewa na kusababisha hata wengine wanaojiheshimu waonekane hawana maana.
Staa wa filamu, Aunt Ezekiel ‘Gwantwa’ anatibua hali ya hewa kutokana na skendo zake za waume za watu pamoja na ile ya kufumwa chumbani akiwa na mchumba wa mtu mwaka juzi.
Aunt alifumwa akiwa na brazameni, Mwilu Mwilola ‘Silvanus’ ambaye alikuwa mchumba wa msanii, Sara Mwakapala. Hivi sasa Aunt na Silva ni wapenzi wa kudumu.
Skendo za Miss Tanzania 2006/07, Wema Isaac Sepetu kubadili wanaume mara kwa mara na ‘kashkash’ za kukamatwa na polisi, ni baadhi ya vitu vinavyochafua ‘statas’ ya ustaa ndani ya ‘Bongoland’.
Mastaa Jacqueline Pentzel, Jacqueline Patrick, Blandina Chagula ‘Johari’, Sylvia Shally, Zuwena Mohamed ‘Shilole’, Elizabeth Michael ‘Lulu’ na wengineo wengi pia wanatajwa kuwa sehemu ya ‘uchafuzi’ wa hali hewa katika tasnia kutokana na skendo zao za hapa na pale.
No comments:
Post a Comment