Hapo mwanzo Mungu aliumba ulimwengu na wanyama wake. Kila mnyama alipewa
miaka ya kuishi 30. Kati ya wanyama walioumbwa walikuwa Punda, Mbwa na
binadamu. Mungu akawauliza wanyama hao Je! unadhani miaka hiyo thelathini
inakutosha? Kila mmoja akajibu hivi:
Punda: Mimi nikae nikitumikishwa miaka 30, niwe kihongo miaka yote hiyo?
Loh! kazi hiyo ni kubwa sana . Mimi nipunguzie iwe miaka 10 tu inanitosha
bwana.
Mungu: Sawa wewe utaishi miaka kumi tu.
Mbwa: Mimi nikae nikilala nje miaka thelathini! Kula majalalani, kubweka
usiku kucha. Naomba unipunguzie niishi miaka kumi tu inanitosha.
Nitajitahidi kwa kipindi hicho kulala nje, kubweka na kulinda usiku kucha.
Watanitumia wapendavyo kunusa madawa ya kulevya, kukamata wanyama nk.
Mungu: Sawa, umri wako utakuwa miaka kumi.
Binadamu: Ha! Miaka 30 tu, nita enjoy nini mimi? Niongezee bwana.
Mungu: Sawa, niliyoipunguza kwa punda na mbwa utaongezewa wewe. Nawe
utaishi miaka sabini (30 + 20 + 20 = 70). Kipindi chako cha miaka 30
utaishi maisha yafaayo binadamu, miaka ishirini inayoongezeka utakuwa na
maisha ya punda, na miaka ishirini inayoongezeka utakuwa na maisha kama ya
mbwa.
Binadamu: Ahsante sana bwana na iwe kama ulivyosema.
Miaka 0 – 30+: Maisha mazuri sana (hayo ndiyo maisha ya binadamu). Maisha
ya kutafuta marafiki, maisha ya kulishwa, maisha ya kuwaandikia barua girl
friends na boy friends, kutafuta pen pal. Maisha ya kuangalia mtindo mzuri
wa nguo, nywele, kutembea kwa mikogo, kutuma message kila dakika,
kupigiana simu kila saa, ugomvi usio na kichwa wala miguu, kujifunza
kuvuta bangi, kunywa pombe, kuhudhuria madisco n.k.
Miaka 35 – 50: (Maisha ya punda). Wengi wanajitegemea wameoa au kuolewa.
Maisha magumu, unapanga chumba lakini mhh kodi sasa watoto watano na mke
chumba kimoja, kibarua wa kubeba zege, kimbiza shilingi, huna muda wa
kwenda disco tena au kuangalia mitindo mipya, hakuna kulala hapa. Watoto
wanasumbua shule, wanaumwa, kadi nyingi za harusi, madeni hadi unawakimbia
marafiki zako. Hii itaendelea hadi upite umri wa miaka hamsini.
50+ tuseme 60: Mstaafu. Unakaa nyumbani, unalinda boma (maisha ya mbwa),
nyumba imebomoka huna pesa ya kurepair, nyumba inavuja, watoto wote
wameondoka wanahangaikia maisha yao na wake/waume zao. Huna jinsi wewe ni
kama mlinzi wa eneo ulilochagua.
Je! Katika maisha haya upo kundi gani? Jiandae hatua unayoendea ni ngumu
zaidi. Jipange, wakati ni huu.
JIPANGE SAWASAWA!!
No comments:
Post a Comment