Usizini ni amri ya saba(7) wala sio ya sita(6), wanaosema ni ya sita wanaikwepa amri ya pili(2) inayokataza kuabudu sanamu.
1. Mimi ni Bwana Mungu wako, niliyekutoa katika nchi ya Misri katika nyumba ya utumwa. Usiwe na miungu mingine ila mimi.
2.Usijifanyie sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu chochote kilicho juu mbinguni, wala kilicho chini duniani,wala kilicho majini chini ya dunia. Usivisujudie wala kuvitumikia; Kwa kuwa mimi Bwana Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu; Nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao, nami nawarehemu maelfu elfu wanipendao, na kizishika amri zangu.
3.Usilitaje bure jina la Bwana Mungu wako, maana Bwana hatamhesabia kuwa hana hatia mtu alitajaye jina lake bure.
4.Ikumbuke siku ya sabato uitakase. Siku sita fanya kazi, utende mambo yako yote; lakini siku ya saba ni sabato ya Bwana Mungu wako, siku hiyo usifanye kazi yoyote, wewe, wala mnyama wako, wala binti yako, wala mtumwa wako, wala mjakazi wako, wala mnyama wako wa kufuga, wala mgeni aliye ndani ya malango yako. Maana kwa siku sita Bwana alifanya mbingu na nchi, na bahari, na vyote vilivyomo, akastarehe siku ya saba; kwa hiyo Bwana akaibarikia siku ya sabato akaitakasa.
5.Waheshimu baba yako na mama yako; siku zako zipate kuwa nyingi katika nchi upewayo na Bwana, Mungu wako.
6.Usiue
7.Usizini
8.Usiibe
9.Usimshuhudie jirani yako uongo.
10.Usiitamani nyumba ya jirani yako, usimtamani mke wa jirani yako; wala mtumwa wake, wala mjakazi wake, wala ng'ombe wake,wala punda wake, wala chochote alicho nacho jirani yako
No comments:
Post a Comment