Friday, January 20, 2012

Hutoamini LAKINI ni kweli

Ona jinsi wadandiaji treni walivyojaa katika treni ya abiria huko Jakarta Indonesia. Ni hatari sana kwa usalama wao lakini hali ya maisha ipo chini na hawana jinsi ya kusafiri. Tanzania hii haipo kabisa. Kweli ukisema kwangu kunaungua ujue kwa mwenzio kunateketea kabisa

Ili kuwazuia hao wadandiaji serikali imeanzisha utaratibu wa kufunga mipira ya chuma inayoning'inia kwa juu ili treni ikipita mipira hio iwabamize wadandiaji kama unavyoona pichani hapo juu

Waone hawa walivyotulia utadhani ni halali yao kukaa hapo juu. Na hapo treni inatembea tena kwa kasi, we angalia pembeni pande zote utaona picha kama imevurugika, hio inatokana na mwendo ambao ni wa kasi sana.

No comments: