WADAU wa muziki wa Injili wa Dar es Salaam, wameipongeza
Kampuni ya Msama Promotions kwa kuamua tamasha la Pasaka kufanyika kwenye
Uwanja wa Taifa badala ya Diamond Jubilee.
Maoni hayo yametolewa na
baadhi ya wadau wa muziki wa Injili waishio Dar es Salaam baada ya kutangazwa
kuwa tamasha la Pasaka litafanyika Aprili 8 mwaka huu Uwanja wa Taifa. "Nikiwa Mkristo mwenye kupenda kusikia ujumbe wa neno la
Mungu pia kwa njia ya uimbaji, nimefurahi sana kusikia tamasha la Pasaka
litafanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam," alisema Jimmy Bukuku wa
Mbagala.
Bukuku anayeabudu Kanisa la
Pentekoste Church of Holiness Mission (PCHM) la Tandika, alisema kwa namna
fulani tamasha hilo litawakuza watu kiroho. Alisema, mbali ya kuburudisha na kufariji, ujumbe wa neno la
Mungu ambao hupatikana kupitia nyimbo, huweza kuwabadili wengi.
Bukuku alisema kutokana na
ujumbe wa neno la Mungu kumgusa kila mwanadamu, ndio maana muziki wa Injili
umekuwa ukiwagusa wengi bila kujali ni Mkristo au Muislamu. Alisema kwa upande wake analiombea tamasha hilo ili
lifanikiwe kwa sababu limekuwa likiwabadili na kuwajenga wengi kiroho.
Alisema analisubiri kwa shauku
tamasha hilo la Pasaka akiamini litakuwa lenye upako kama yaliyowahi kufanyika
chini ya Msama Promotions. Mdau mwingine aliyegusia tamasha hilo, ni Furaha Masinga wa
Kanisa la Mchungaji David Mwasota ambaye kwa upande wake, alisema litasaidia
wengi kuimarika kiroho.
|
No comments:
Post a Comment