Wednesday, February 15, 2012

Wakazi huko Syria wakimbia mashambulizi ya vifaru

Wakazi wa mji wa Idlib uliopo Kaskazini-Magharibi mwa nchi hiyo wakikimbia vifaru vya serikali vilivyokuwa vilivyokuja kuwaangamiza jana Feb 14, 2012. Bado Rais Bashar Al-Asad anasema yeye haagizi jeshi kuua raia wake. Ni ujeuri usio kifani. Urusi na China ni chi zinazomuunga mkono. 
Hapa wakiingia kwenye kibasi japo waende eneo lenye usalama huku askari wa jeshi alieasi (Syrian Free Army) akiwapa ulinzi

Hivi ndio vifaru vyenyewe vikiwa tayari kuangamiza mali na kila mtu wanaeamini yupo kinyume na msimamo wa Rais Bashar Al-Asad

Ona jinsi ambavyo watoto wanalia na wazazi (wa kike) wakiwa wamekata tamaa. Kweli fujo au vita ikitokea wanaoteseka ni AKINA MAMA NA WATOTO.
Pilika za kukimbia mashambulizi. Enyi nchi zenye amani endeleeni kumshukuru Mungu kwa amani mliyonayo.

No comments: