Wednesday, March 28, 2012

Mradi wa Maji wa Vodacom kunufaisha wanakijiji 4,000 Dodoma

Mkazi wa kijiji cha Inyumbu Mkoani Dodoma Bw.Samwel Chindombwe akisalimiana na Mkuu wa Mfuko wa kusaidia jamii wa Vodacom Tanzania(Vodacom Foundation) Yessaya Mwakifulefule,baada ya kukabidhi msaada wa mradi wa maji wenye thamani ya shilingi milioni 40 katika kijiji hicho

Mkuu wa Mfuko wa kusaidia jamii wa Vodacom Tanzania(Vodacom Foundation) Yessaya Mwakifulefule.(kulia )akiwa na wakazi wa kijiji cha Inyumbu Mkoani Dodoma wakinywa maji salama yaliyotokana na mradi wa Kisima kilichojengwa na Vodacom ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa mradi huo wenye thamani ya shilingi milioni 40 uliotolewa na Vodacom Foundation

Mkuu wa Mfuko wa kusaidia jamii wa Vodacom Tanzania(Vodacom Foundation) Yessaya Mwakifulefule,akimtwisha Amina John ndoo ya maji ya kunywa yaliyochotwa katika kisima kilichotolewa msaada na Vodacom Foundation kwa ajili ya wakazi wa kijiji cha Inyumbu Mkoani Dodoma,Mradi huo umegharimu thamani ya shilingi milioni 40.

Baadhi ya wakazi kijiji cha Inyumbu Mkoani Dodoma waliohudhuria sherehe ya uzinduzi wa kisima cha maji salama uliojengwa na Vodacom Foundation.

Hapa wakichota maji kwenye bomba mara baada ya mradi huo wa maji kuzinduliwa rasmi.

Wakazi wa kijiji cha Inyumbu Mkoani Dodoma wakicheza wakifurahia mara baada ya kukabidhiwa visima vya maji

Visima vyenyew vya maji ndio hivi hapa

No comments: