BLOG YETU

This blog is for critical thinkers, people with open mind, ready to accept criticisms and work on them. Sharing the know-how, skills and experiences of Life and Technology at large. You are warmly welcome!! ---------------------------------------------------- Blogu hii ni kwa ajili ya wenye fikra makini wapendao kupokea na kufanyia kazi ukosoaji. Walio na mtazamo chanya tena mpana katika kushirikishana maarifa, ujuzi na uzoefu wa maisha na teknolojia kwa ujumla wake. Karibuni sana !!!

Monday, April 9, 2012

Je, Ni Nani Anayemfariji Msichana Huyu Wa Miaka 18 Aliyeondokewa Na Mpenzi Wake?


Ndugu zangu, 
NI kazi ngumu kuwa wakili kwa anayeonekana na jamii kuwa ni 'shetani'. Lakini, kwenye hili la kifo cha kusikitisha cha msanii Steven Kanumba kuna haja ya kukaa chini na kutafakari kwa bidii.
 
Kuna maswali pia ya kujiuliza juu ya msichana huyu wa miaka 18 ambaye sehemu kubwa ya jamii imeshamuhukumu kuwa ni muuaji.
Kuna hata ambao hawalijui jina lake la kamili, bali, anajulikana kama 'Lulu'.  Jina lake ni
Elizabeth Michael.
 
Simulizi ya Lulu inaonyesha kuwa yeye na Kanumba walikuwa na mahusiano. Na wivu pia umeingia kwenye mahusiano yao. Hivyo basi, ugomvi na hatimaye kifo cha Kanumba.
Uchunguzi kamili haujakamilika. Na kama haujakamilika, basi, Lulu anabaki kuwa ni mtuhumiwa na si muhusika na kifo hicho. Kumwita Lulu muuaji  ni kuharakisha kutoa hukumu isiyo ya haki. Pamoja na machungu yetu, lakini wanadamu tunapaswa kuwa na subira.
Na ukweli unabaki, kuwa Lulu ni mwanadamu kama wewe na mimi. Na kwa yote yaliyotokea, anabaki kuwa ameondokewa na mpenzi wake. Je, ni nani anayemfariji msichana huyu wa miaka 18 aliyeondokewa na mpenzi wake?
Maggid Mjengwa, 
Dar es Salaam. 
0788 111 765
http://mjengwablog.com



Posted by Daudi Mlaule at 9.4.12

No comments:

Post a Comment

Newer Post Older Post Home
Subscribe to: Post Comments (Atom)

About Me

Daudi Mlaule
View my complete profile

Other Blogs/Blogu Zingine

  • AY-Ambwene Yessaya
  • Bongo5
  • BongoCelebrity
  • Dada Chemi
  • Injili
  • Jiachie
  • Kita Ngoma
  • Michuzi
  • Mzee wa Sumo-Bukuku
  • SpotiStarehe

Zilizowekwa-Facebook

Daudi Mlaule anakwambia "Tazama Picha Hizi"

Designed by Mlaule DJ

Copyright 2008-All rights Reserved
Powered By Blogger
Theme images by Jason Morrow. Powered by Blogger.