Saturday, May 5, 2012

SPIKA ANNE SEMAMBA MAKINDA AWA MGENI RASMI KILELE CHA MAADHIMISHO YA ALBINO MKOANI LINDI

Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda (Mb) akipata maelezo kutoka kwa Ndg. Abdalah Omar kutoka Chama cha Albino Tanzania juu ya matumizi ya mafuta maalum ya ngozi kwa ajili ya watu wenye ulemevu wakati alipotembelea mabanda ya maonesho ya bidhaa na huduma mbalimbali za watu wenye ulemavu wa Ngozi. Spika alikuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya saba ya siku ya Albino yaliyofanyika kitaifa Mkoani Lindi Jana.

Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda (Mb) akipokea DVD maalumu kuhusu Albino na Maisha yao kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa shirika lisilo la kiserikali la Under the Same Sun Bi. Vicky Mtetema wakati wa maadhimisho ya  Siku ya Albino yaliyofanyika Lindi. Shirika la ni mdau mkubwa wa watu wenye ulemavu wa Ngozi na linajishughulisha na kutoa elimu kwa watu wenye Ulemavu wa Ngozi pamoja na Misaada mbalimbali. Spika walikuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya saba ya siku ya Albino yaliyofanyika kitaifa Mkoani Lindi Jana.

Dk. Mashingo Lerise kutoka Taasisi ya Magonjwa ya Ngozi na Saratani (Ocean Road) akimweleza Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda (Mb) juu ya huduma mbalimbali zitolewazo na taasisi hiyo kwa watu wenye ulemavu (Albino) baada ya Mhe. Spika kutembelea banda lao wakati wa kilele cha Siku ya Albino kitaifa iliyofanyika Lindi. Kulia ni baadhi ya madaktari wa saratani ya Ngozi kutoka taasisi hiyo katika Hospitali za KCMC na Mkoani Lindi.

Mhe. Spika akioneshwa mojawapo ya mafuta maalumu ya kuzuia Mionzi ya Jua ambayo hutolewa bure na serikali kupitia  tassisi ya magonjwa ya Ngozi kwa watu wenye ulemavu wa Ngozi.

Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe. Ludovick Mwananzila, Spika wa Bunge  Mhe. Anne Makinda, Mweneyikiti wa Chama cha albino Tanzania Ndg. Ernest Kimaya, na Kamishna wa Ustawi wa Jamii kutoka wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Ndg. Danford Makala wakipokea maandamano wakati wa kuadhimisha siku ya Albino Mkoani Lindi ambapo Spika alikuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya saba ya siku ya Albino yaliyofanyika kitaifa Mkoani Lindi Jana.

Waandamanaji wakipita mbele ya Jukwaa kuu

Bi. Zakia Matimbwa kutoka Albino Revolution Cultural Troup cha Dar es Salaam akighani Ngonjera iliyobeba ujumbe wa kulaani mauji ya Albino wakati wa katika maadhimisho ya saba ya siku ya Albino yaliyofanyika kitaifa Mkoani Lindi jana

Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akiwahutubia wananchi wa Mkoa wa Lindi wakati wa maadhimisho ya saba ya siku ya Albino yaliyofanyika kitaifa Mkoani Lindi jana. Mhe Spika alikuwa Mgeni rasmi katika kilele hicho.

No comments: