As you may know I have twins McNathan & Mirabel; mimi na familia yangu tunaishi Tabata-Liwiti.
Tulikuwa
na wasichana wawili wa kazi na mmoja aliondokaga akabaki mmoja; hivyo
tukawa ktk harakati za kutafuta potential replacement ili wawe wawili.
Here comes the story part I.
Jana
21.08.2012 nlipotoka job, wife alinipa taarifa kuwa mdogo wangu wa kike
(mwenye salon ya kike kimanga) alimpigia simu kuwa amepata msichana na
atakuja nae home jioni akifunga saluni.
Ikabidi nimpigie simu mdogo wangu ili anipe full information.
Mdogo
wangu akanimbia majira ya jioni uyo msichana alifika Saluni kwake
akidai anatafuta kazi za ndani. Uyo msichana akasema yeye alikuwa
anfanya kazi morogoro but ametoroka kwani alikuwa anateswa na mama
mwenye nyumba.uyo msichana akizidi kuongeza kuwa yeye hana mawasiliano
ya ndugu yeyote ila baba yake anishi mwanza but hanjui mama yake. Basi
mdogo wangu akamuonea huruma akamkaribisha saluni ilia je nae home jioni
na nifanye nae mahojiano ya kina.
Jana
majira ya saa 3 usiku baada ya wao kurejea home na kula chakula ikabidi
nianze kumhoji yule binti.Akanitajia jina lake na umri wake 15yrs, na
nia yake ni kufanya kazi za ndani na akipata pesa ataenda kwao kusalimia
then angerudi tena kuendelea na kazi yake.
Ni binti mdogo na nilitamani kumsaidia.
Baada
ya kupata maelezo kutoka kwake; nilimuambia kwa sababu hatumfahamu ni
lazima tukatoe report kwa balozi/mjumbe kabla hajaenda kulala na
alikubali.
Nikaenda
kwa mjumbe akawa ameshalala; ikabidi nimwambie wife kesho asubuhi
(yaani leo) wakiamka waende kwa balozi/mjumbe kutoa taarifa na
kuandikishana.
Leo asubuhi najiandaa kwenda kazini; kumbe yule binti ametoroka mapema asubuhi after mlango na geti kufunguliwa. Majirani
wakasema walimuona katoka na viatu mkononi wakazani anaenda kutupa taka
coz alikuwa anafagiafagia nje. Kuangalia vitu sebuleni na chumbani kwa
kina dada ikaonekana everything is OK.
Basi nikawmambia mdogo wangu na kijana flani wa jirani wamfuatilie then mimi nikaondoka zangu kuelekea job.
Here comes the story part II.
Majira ya saa 4 asubuhi nikiwa job nilimpigia simu mdogo wangu anitaarifu yaliyojiri:
Akaniambia
yule binti walimuona na akakimbilia nursery school flani karibia na
barakuda na kwa msaada wa raia wengine walimkamata.Walimpiga kidogo na
kumsachi. Walimkuta na elfu 90 na alikiri kuwa aliziiba ktk wallet ya
mdogo wangu. Ikabidi mdogo wangu achukue bodaboda wakaenda nae hadi
saluni kwake kimanga ili akamhoji zaidi.
Yule
binti akasema kuwa alitudanganya hajatokea morogoro but anaishi na bibi
ake mbagala na ule ndo mchezo wake yeye na bibi yake.
Akasema
kuwa bib ake ni mchawi na huwa anamtumaga kwa nyumba za watu kwa mbinu
ya kuomba kazi but baadae wanaiba na kuchukua watoto wadogo kimazingara.
Akaongeza kuwa hao watoto wadogo huwa wanawachukua misukule na wengine wakiwa wakubwa wanatumwa kama alivyotumwa yeye.
Yote hayo aliyasema bila woga huku watu wakiwa wamemzunguka pale saluni.
Akasema
kuwa jana alipoingia getini bibi ake alikuja kimazingara but ghafla
macho yake yalianza kumuwasha na hakuwa na amani. Kuona vile bibi ake
akaondoka.
Ilipofika
muda wa kulala alienda kuoga but aliporudi chumbani alimkuta mdogo
wangu anasali ndipo alipigwa na miale ya blue na nyekundu akakimbia
kurudi sebuleni.
Aliporudi sebuleni alimkuta wife anachek TV nae wife akashtuka kumuona yule binti hana amani.
Baade yule binti akaenda kulala ndipo wife akachukua maji ya Baraka akanyunyiza pale mlangoni na sebuleni kisha akaenda kulala.
Yule
binti akazidi kuelezea kuwa usiku hakulala kwani aliteseka sana na
kuweweseka na bibi ake alipokuja kimazingara hawakuweza kuchukua watoto
ikabidi aondoke na kumuacha yule binti kwani alikuwa kaishiwa nguvu.
Akasema
tangu aanze iyo kazi hajawahi kukamatwa na akmeshangaa sisi tumeweza
kumkamata na kueleza siri zake. Akasema bibi ake alimjia kimazingara na
akamwambia asirudi kwake kwani ametoa siri.
Alionesha CHALI alizochanjwa na bibi ake kama kinga na alipokuwa anapigwa hakusikia maumivu yoyote.
Alielezea
mambo mengi ambayo mdogo wangu hakuweza kunielezea ktk simu kwani nae
alikuwa anatetemeka kutoamini yaliyoukuwa yanatokea. Walimuachia
akaondoka zake.
I felt so sorry for my twins but I thank GOD wamebaki salama.
Tuwe makini sana na wasichana wa kazi ndugu zangu; you may share it to your relatives and beloved.
Alex N. Mero
No comments:
Post a Comment