Friday, November 14, 2008

Vipindi vya enzi hizo vya RTD unavikumbuka?

Wadau leo nimeona nije na hii nyingine, nimekumbuka sana ile miaka ya nyuma kidogo wakati tulikuwa hatuna radio stations nyingi kama zilivyo sasa, wakati huo station ilikuwa ni Radio Tanzania tu na ile idhaa yake ya kiingereza (External).
Fashion ya radio ilikuwa ni zile wanaita RADIO MKULIMA na brand names zake zilikuwa ni NATIONAL Panasonic ama PHILIPS. Mzazi alikuwa anainunua RTC (yale maduka ya uma).Tukirudi katika vipindi, navikumbuka sana vipindi vifuatavyo ambavyo bila shaka mdau utakubaliana na mimi vilikuwa maarufu kutokana na zile nyimbo za utangulizi kuashiria kipindi kuanza ama kumalizika.
"Sikiliza Bwana Umeme... (Bwana Umeme) - Kile kipindi cha TANESCO cha kuelimisha umma kuhusu matumizi mazuri ya umeme.
"Starehe na BP " - Uncle J. (Julius Nyaisanga) alikuwa anakimudu vyema kabisa""Kahawa ni Mali" - Namkumbuka sana yule mama wa kiashirio cha kipindi akitamka hayo maneno kwa rafudhi ya kichaga.
"Jifunze Kiswahili Fasaha" - sina uhakika kama nimeandika vyema tittle yake lakini kilikuwa ni kile kipindi kizuri kilichobuniwa kuhamasisha watu kuzungumza kiswahili katika harakati ya kuwaunganisha watu wa mikoani na wa Bara. Nakumbuka kiashirio chake kuna sehemu inasema.. na mikoani... ni kiswahili chatumika.....Bila kusahau vipindi kama..
"TTCL Simu kwa Maendeleo" kipindi cha "Serikali za Mitaa", " Afya yako /Afya ya jamii " sikumbuki vyema title ila nakumbuka kiashiria cha kipindi ulikuwa ni wimbo mmoja anaimba Kept John Komba na kundi lake wakati ule.
Ukija vipindi vya week ends kama "Club Raha leo Show", bila kusahau kipindi cha "Mama na Mwana" namkumbuka mtangazaji Edda Sanga alikuwa anakimudu vyema kipindi na zile hadithi za "Adili na Nduguze", "Kisa cha Mfalme Juha", ile hadithi ya watoto wa mfalme wanakwenda kutafuta wachumba wa kuoa... n.k wadau ongezeeni hapo kumbukumbu zenu.
Japokuwa kilikuwa ni kipindi cha watoto lakini nakumbuka watu wazima walikuwa wanazifuatilia kwa umakini sana zile hadithi bila kukosa sehemu hata moja juma moja baada ya lingine.
Wakati ule radio ilikuwa na msaada mkubwa kuelimisha jamii nzima (wakulima, wafanyakazi, wafanyabiashara) kuhusu mambo mbali mbali na watu walikuwa wanafuatilia sana.

Je, wewe mdau unakumbuka nini miaka hiyo hapo kunako Radio Tanzania (RTD)???

No comments: