Friday, March 4, 2011

BABY MADAHA aanika siri zake za chumbani

Msanii wa muziki wa kizazi kipya ambaye pia amejikita katika uigizaji wa filamu, Baby Joseph Madaha hivi karibuni ameanika siri zake za chumbani huku akidai kuwa, anafanya hivyo kutokana na jinsi mapenzi yanavyochukua nafasi kubwa katika maisha yake.

Akizungumza na Ijumaa katika mahojiano maalum juu ya maisha yake ya kimapenzi, msanii huyo alisema kuwa, yeye kama mtoto wa kike amekuwa akijitahidi kuwa mtundu faragha lengo likiwa ni kuhakisha haachwi na mpenzi wake.

“Unajua asilimia kubwa ya maisha yangu imeshikiliwa na mapenzi, hivyo nahakikisha najipa furaha kwenye uwanja huu. Nampenda sana mpenzi wangu wa sasa hivyo nafanya kila ninaloweza kuhakikisha simkosi.

“Najua amedata na jinsi nilivyo, midomo yangu, macho yangu na kifua changu, pia nadhani yale ninayomfanyia tuwapo faraha yanamchanganya.

“Napenda mengi anayonifanyia, anaponishika kiuno nikiwa katika mavazi ya ndani yenye rangi nyekundu au nyeusi, ‘anaponikisi’ na kunikumbatia lakini pia katika mambo yetu yaleee, ni mtundu sana, kwa kweli nampenda,”alisema Baby Madaha ambaye kwa sasa inadaiwa anatoka na mtoto wa kigogo mmoja (jina tunaminya kwa sasa)

No comments: