Tuesday, February 7, 2012

Bwawa lapasuka na kusababisha mafuriko yaliyouwa wa 8 huko Bulgaria

Gari likiwa limegharikishwa mbele ya nyumba iliyoharibiwa na mafuriko hayo katika kijiji cha Biser huko Bulgaria jana Jumatatu Februari 6, 2012. Katika watu 8 waliokufa wanne kati yao walikutwa na maji wakiwa ndani ya nyumba na wakashindwa kutoka, kina cha amaji kilifikia mita 2.5 na maji yalikuwa baridi sana na hadi barafu pia. Pole sana kwa walioathiriwa na mafuriko hayo.

Mtu huyu akikagua mabaki ya nyumba yake kama anaweza kupata chochote cha kumfaa. Kijiji cha Biser kipo maili 180 mashariki mwa mji mkuu Sofia.

Mtaa wote maji, nyumba , magari na mali zingine zimeharibiwa sana.

No comments: