Tuesday, February 7, 2012

WAISLAMU WA ARUSHA WALAANI MAGAIDI WA BOKO HARAM WA NIGERIA





 . Katika hatua nyingine, aliwataka wananchi kuheshimu viongozi waliopo madarakani na kuacha kupinga kila kitu kinachotamkwa na kiongozi aliyeko madarakani, badala yake watoe mchango wakusukuma maendeleo ya taifa hadi utakapo fanyika uchanguzi mwingine. Naye Sheikh mkuu wa Ahamadiyya kanda ya kaskazini, Mzafara Ahamad,alisema kuwa lengo lakongamano hilo lililowashirikisha viongozi mbalimbali wa madhehebu ya dini ya kiislamu nchini ni kutoa mada ya kuomba amani na kulaami mauaji ya kikatili yanayoongozwa na kikundi haramu cha kiislamu nchini Nigeria. Alisema kuwa kongamano hilo lilienda sanjari na uzinduzi wa msikiti huo wa Ahmadiyya Muslim Jamaint uliogharimu kiasi cha shilingi milioni 70 kwa ajili ya ukarabati ulioanza mwishoni mwa mwaka jana . Kwa upandewa sheikh mkuu wa Ahamadiyya mkoa wa Morogoro,Bakari Kaluta,aliwataka viongozi wa dini nchini kutawala kiuadilifu huku wakiongozwa na mwenyezi mungu katika mahubiri yao na kuacha kuwa sehemu yakuleta mitafaruku ya kidini . Ameyasihi madhebebu ya dini kuwa na utaratibu wa kuandaa makongamano ya kuomba amani,kwani bila hivyo nchi itaelekea kubaya kwakuwa baadhi ya viongozi wa dini wamekuwa wakitumia vibaya maandiko matakatifu kwa kuhubiri uvunjifu wa amani kwa maslahi yao binafsi. Naye meya wa jiji la Arusha ,Gaudence Lyimo aliyekuwa mgeni rasmi katika kongamano hilo,aliyasifu madhehebu ya dini ya kiislamu kwa kuandaa kongamano hilo la kuomba amani ,aliwatia moyo viongozi hao kuwa serikali inatambua mchango wao na inawaungamkono kwa jambo hilo. Aliwasihi viongozi hao wa dini kuwa sehemu ya serikali katika jitihada zake za kuhakikisha kuwa amani inapatikana kwa kila mtu hapa nchini na duniani kote.

No comments: