Saturday, February 4, 2012

KIWANDA CHA MAGODORO CHA "PAN AFRICA" CHATEKETEA KWA MOTO TEMEKE DSM.

Askari wa vikosi vya kuzima moto wakiwa kazini wakati walipokuwa wakizima moto kiwandani hapo

Hiki ndiyo kiwanda chenyewe kama kinavyoonekana kikiwa kimeteketea kabisa

Magari ya vikosi vya kuzima moto yakiwa yamejipanga katika kiwanda hicho yakiendelea na kazi ya kuzima moto

Askari wa kikosi cha kuzima moto wakizima moto huo

Kamanda Misime wa kanda ya kipolisi Wilaya ya Temeke akihojiwa na waandishi wa habari mara baada ya kusimamia zoezi la kuzima moto katika kiwanda cha magodolo cha Pan African kilichopo Chang'ombe jijini Dar es salaam
kiwanda hicho kimeteketea kabisa kwa moto  kutokana na mlipuko uliotokea kwenye mashine za kunolea visu vya kukata magodoro kiwandani hapo, Kamanda Misime amesema hakuna taarifa ya mtu yeyote kupoteza maisha wala kujeruhiwa katika tukio hilo la moto
Watu mbalimbali wakiangalia tukio hilo

Hawani baadhi raia wa kigeni ambao ni wafanyakzi wa viwanda vya jirani na kiwanda hicho

No comments: