Wednesday, March 21, 2012

Ajali mbaya la basi la Prince Muro iliyotokea usiku maeneo ya Senjele likielekea Tunduma.


Ajali mbaya la basi la Prince Muro iliyotokea usiku maeneo ya Senjele likielekea Tunduma. Mwendo kasi ndio chanzo cha ajali hiyo mmoja Afariki 14 majeruhi

Basi la Price Muro Baada ya kupata ajali usiku wa kuamkia juzi likielekea Tunduma kutokea Dar es salaam.

Likiwa linaonekana baada ya kupinduka 

Hivi ndivyo zinavyo onekana Damu na viti kuharibika vibaya baada ya ajali hiyo iliyo tokea majuzi usiku

Baadhi ya mabaki ya vitu baada ya ajali hiyo juzi usiku

Hili Ndilo Gari la mizigo ambalo basi la Price muro lilitaka kulipita, na  baadae kushindwa na kupinduka baada ya kukutana na Gari lengine mbele yake


Shimo hili limechimbika wakati wa ajali hiyo ilipo tokea juzi usiku

Hapa ndipo Basi la Prince Muro lilipo taka kuingia na kulikwepa gari hili na kupindukia upande wa pili 

Muonekano wa gari hili la mizigo ambalo limeharibikia barabarani 

Mmoja wa majeruhi ambae alikuwa anatokea Dar es salaam kwenda kuwasalimu ndugu zake Ileje aliye fahamika kwa jina moja tuu la Andendekisye akiwa katika Hospital ya Ifisi Mbeya

Baadhi ya Majeruhi walio nusurika katika ajali hiyo wakiwa katika Hospitali ya Ifisi kuelekea katika matibabu na kutazamwa kama wamepata matatizo yoyote.

Hawa ni majeruhi kati ya wale 14

Mganga mkuu wa Hospitali ya Ifisi Dkt. Mbilinyi akiongea na moja ya majeruhi wa ajali hiyo.

Majeruhi ambao wamenusurika katika ajali hiyo mbaya wamesema kwamba dereva huyo alikuwa mwendo kasi tangia walipo fika mikumi, Wameendelea kudai kwamba walimpa onyo mala kadhaa lakini hakuweza kuwasikiliza na akaongeza mwendo kasi zaidi mpaka walipo pata ajali hiyo maeneo ya Senjele kuelekea Tunduma.
Habari kamili itakuja mpaka sasa kuna majeruhi 14 na mtu mmoja amefariki Dunia

No comments: