Wednesday, March 21, 2012

Imani inaweza kuwa kitu KIZURI au KIBAYA kabisa!

Muumini huyu ambaye humuomba "Nino Fidencio" amfanyie miujiza, hapa akisaidiwa na wenzake kuzama kwa mara nyingine katika lindi la TOPE huko El Espinazo katika jimbo la Nuevo Leon nchini Mexico juzi Machi 19,2012. Maelfu ya waumini hao humuomba raia maarufu wa Mexico aitwaye "Nino Fidencio" miujiza kwa njia ya kujizamisha katika tope. Wanaamini "Mganga wa Kienyeji" huyo huweza kutibu watu viungo ndani ya mwili bila kufanya upasuaji wala kumdunga mtu sindano za usingizi. Nino Fidencio alishafariki dunia tangu 1938 lakini wao wanaamini anatibu hadi leo. Du ukistaajabu ya Musa utaona ya Firauni!

Muumini akiwa ameibuka toka katika TOPE hilo, aisee si kila imani ni njema, ichunguze kabla hujajiunga nayo!

Mwingine ni huyu hapa akisaidiwa kuzama katika tope hilo, Imani ni kitu kingine kwasababu tope hili lina uchafu mwingi tu ambao unaweza kuleta maradhi hatari sana kwa wanaozama humo.

No comments: