Thursday, March 1, 2012

BREAKING NYUZZZZZ: MELI YA MV. MAENDELEO YENYE KUFANYA SAFARI ZAKE KATI YA UNGUJA NA PEMBA YAKWAMA MAJINI ASUBUHI HII

TAARIFA ILIYOIFIKIWA GLOBU YA JAMII HIVI PUNDE,INAELEZA KUWA MELI YA MV. MAENDELEO INAYOFANYA SAFARI ZAKE KATI YA UNGUJA NA PEMBA IMEKWAMA ASUBUHI HII NJE KIDOGO YA BANDARI YA PEMBA (MITA KAMA 180) WAKATI IKIJIANDAA KUPAKI KATIKA BANDARI YA PEMBA ILI ABIRIA WALIOPO NDANI YA MELI HIYO WAWEZE KUSHUKA.
KWA MUJIBU WA NAHODHA WA MELI HIYO NA MDAU AMBAYE YUPO NDANI YA MELI HIYO ANAELEZA KUWA CHANZO CHA KUKWAMA KWA MELI HIYO NI KUTOKANA NA BOYA ZINAZOKUWEPO KWENYE BANDARI HIYO KWA AJILI YA KUELEKEZA MELI SEHEMU YA KUPITA ILI KWENDA KUPAKI,ZILIKUWA ZIMEHAMA KATIKA MAENEO YAKE KUTOKANA NA UPEPO MKALI ULIOZISUKUMA KUTIKA ENEO HILO NA KUPELEKWA ENEO LINGINE.
MPAKA SASA HAKUNA MADHARA YEYOTE TOKEA,KWANI TARATIBU ZA KUINASUA MELI HIYO MAHALI HAPO INAENDELEA HIVI SASA,HUKU ABIRIA WOTE WAKIWA BADO HAWAJASHUMA MELINI HUMO.
GLOBU YA JAMII INAENDELEA KUFUATILIA KWA MAKINI TUKIO HILO NA TUTAENDELEA KUPEANA TAARIFA KADRI ZITAKAVYOKUWA ZIKITUFIKIA.

No comments: