Thursday, March 1, 2012

HALI KILWA RODI SI SHWARI, HATUA ZA HARAKA ZINAHITAJIKA

Barabara imejengwa chini ya KIWANGO, na ndio maana Waziri Magufuri aliwaambia waJapan waliotusaidia kuijenga kwamba LAZIMA WAIRUDIE KUJENGA. Sio kwa vile ni msaada basi hata kiwango kiwe chini, alaah!

Hii ndio hali halisi ya Barabara ya Kilwa ya Jijini Da es Salaam kama ilivyokutwa na kamera ya Blogu hii muda si mrefu. Hali hii inafuatia mvua zilizopiga hodi usiku wa kuamkia leo.

Mfereji umebomoka na kuna hatari ukasogea hadi barabarani Hatari..!

 Daraja nalo limepata mushkeri na lami kuchimbika. Kazi ipo...!

 Hebu malizia hiyo sentensi katika hilo daladala unaloliona, hapa ni makutano ya Barabara ya Kilwa na ile ya Kichangani, nayo hayako salama.

Si magari tu, hata waenda kwa miguu nao wako hatarini kuvunjika miguu!

No comments: