Friday, March 30, 2012

HIVI NDIVYO DARAJA LA KIGAMBONI LITAKAVYOKUWA

Mchoro unaoonesha jinsi daraja la Kigamboni jijini Dar es salaam litavyokuwa baada ya kukamilika. Daraja hili, ambalo linajengwa na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) linatarajiwa kuleta chachu kubwa katika ujenzi wa mji mpya wa Dar upande wa pili wa ghuba ya Kigamboni.

China Railways Construction Engineering Group kwa ushirikiano na China Major Bridges ndio walioshinda zabuni ya kujenga daraja hili lenye urefu wa mita 680 lenye njia sita kwa gharama za TSh 214.6. Ujenzi utachukuwa miezi thelathini na sita.Kukamilika kwa barabara hii kutaleta maendeleo na kwa kiasi kikubwa litapunguza gharama za maisha kwa wakaazi wa Kigamboni. Mbunge wa Kigamboni Dkt Faustine Ndugulile ametoa pongezi kwa Wizara ya Ujenzi kufanya shughuli zake za msingi kwa vitendo.

Pia ameipongeza NSSF kwa kufanikisha mchakato huu kuanza kwa kutoa asilimia 60 ya gharama hizi, akisema ushiriki wa NSSF ni mfano mzuri wa ushirikishaji wa sekta binafsi (PPP).

Wadau wakiwa karibu na bango la mchoro wa daraja la Kigamboni wakati wa mechi ya kutafuta mshindi wa tatu wa michuano ya kombe la NSSF 2012 uwanja wa TCC Chang'ombe ambako mfuko huo unaoongoza wa jamii umeandaa mashindano kwa timu za netiboli na soka za vyombo vya habari yanayotarajiwa kufikia kilele siku ya Jumamosi hii.

No comments: