Tuesday, March 6, 2012

UKOMBOZI UNA GHARAMA, HATA YA DAMU

Wanaume wa Libya wakiwa wamebeba majeza ya ndugu zao wakienda kuwazika upya. Watu hao walifukuliwa katika kaburi la pamoja huko Bin-Jawad na waliuawa na majeshi ya Gaddafi wakati wa harakati za kumng'oa. Miili 155 ya waasi (Ambao sasa ni Watawala) ilizikwa huko Benghazi mashariki mwa Libya. Kaburi hilo ndilo lililokuwa kubwa kuliko yote lilipatikana wakati wa mapambano hayo ya kumng'oa Gaddafi, na kweli aling'olewa na kuuawa Octoba mwaka jana. Mazishi hayo yamefanyika jana Jumatatu Machi 5, 2012.

Mama huyu akilia kwa uchungu mkubwa huku ameshika picha ya ndugu yake alikufa katika mapambano hayo.

Wanaume hawa wakiswalia na kuombolezea ndugu zao waliofukuliwa katika kaburi la pamoja huko Bin-Jawad Libya. Takriban waasi 160 waliuawa katika mji huo na majeshi ya Muamar Gaddafi wakati wa mapambano makali ya kumng'oa Gaddafi

Binti mdogo akionyesha kidole kwa mmoja wa watu aliowatambua na ambaye aliuawa katika mapambano hayo, huzuni sana

Wana-Libya hawa wakiwazika UPYA ndugu zao waliofukuliwa katika kaburi la pamoja huko Benghazi ambao waliuawa wakati wa mapambano ya kumtoa Dikteta Muamar Gaddafi.

Mwana Libya huyu akimuombea ndugu yake aliyeuawa katika mapambano hayo ya ukombozi-UKOMBOZI UNA GHARAMA

No comments: