Monday, April 23, 2012

JACOB ZUMA AOA MKE WA SITA, NI BONGI NGEMA

Rais Jacob Zuma na mkewe Bongi Ngema wakikata keki.

...Wakiwa na nyuso za tabasamu.

...Hapa ni wakati wa ndoa ya kimila.

Zuma akiwa amevaa ngozi ya chui na kubeba ngao wakati wa harusi ya kimila.…
RAIS wa Afrika Kusini, Jacob Zuma, jana Jumamosi ameoa mke wa sita katika sherehe ya siku ya pili iliyopambwa kwa shamra za kabila la Wazulu. Rais huyo mwenye umri wa miaka 70 alimwoa Bongi Ngema siku ya Ijumaa katika mvumo wa nyimbo za Kizulu akiwa amevaa ngozi ya chui na kubeba ngao huku akiwa amezungukwa na wanaume waliokuwa wamvalia nguo za wapiganaji wa kijadi.
Msimamizi wa ndoa hiyo alikuwa ni mke wa nne wa Zuma aitwaye Nkandla katika sherehe iliyofanyika KwaZulu-Natal na kufuatiwa na sherehe za kisasa ambazo zilikuwa ni pamoja na kukata keki.
Zuma na Ngema wana mtoto wa miaka saba wa kiume. Ndoa hiyo ni ya tatu katika miaka minne iliyopita naya pili tangu ashike urais wa nchi hiyo mwaka 2009 akiwa rais mwenye wake wengi.
Kiongozi huyo ameoa mara sita na ana watoto 21 ambapo mmoja wa wake zake amekufa na mwingine ambaye ni Waziri wa Mambo ya Ndani, Nkosazana Dlamini-Zuma – ametalikiana naye. Wanawake hao hufaidika kwa kusafiri na rais huyo na kufanya kazi za ukatibu mahsusi, pamoja na kufuatana naye katika ziara za kiserikali.
Pamoja na kwamba Zuma aligharimia ndoa hiyo yeye mwenyewe, serikali pia imeongeza bajeti yake maradufu kwa zaidi ya Dola milioni mbili kutokana na kumwoa mwanamke huyo akiwa mmoja wa familia yake.
Hata hivyo, ndoa ya wanawake wengi inaonekana kupoteza umaarufu nchini Afrika Kusini ambapo ustaarabu wa nchi za Magharibi unazidi kuota mizizi ambapo idadi kubwa ya watu wa nchi hiyo hawakubaliani na utamaduni huo hivi sasa.

No comments: