Friday, April 20, 2012

JINSI FILIKUNJOMBE ALIVYOTOA MAKALI KUHUSU UONGO WA WAZIRI WA FEDHA BUNGENI.Mbunge wa Ludewa kupitia CCM Deo Filikunjombe April 19 2012 bungeni 104.4 Dodoma ameamua kutoa ya moyoni kuhusu waziri wa fedha wa sasa wa Tanzania Mustapha Mkulo.

kwa kuanza Filikunjombe amesema “waziri wetu wa fedha sio muaminifu, na aliesema sio mwaminifu ni CAG na ametajwa humu ndani kwenye ripoti hii, kila mbunge ana hii ripoti na akisoma vizuri ataona madudu ambayo huyu waziri anafanya na ndio maana ilifika wakati fulani hapa ndani miezi kadhaa iliyopita tulibishana sana kuhusu ubinafishaji Mashirika ya Umma ambapo waziri alileta muswada kutaka shirika hodhi la mashirika ya umma CHS liuwawe ambapo wabunge tuliotumwa na wananchi tulipigania, tulitetea lakini waziri huyo kumbe alikua na maslahi yake binafsi”

Filikunjombe amefungua sentensi nyingine kwamba “alitaka liuwawe kwa sababu yeye anataka kuchukua zile mali pamoja na mawaziri wenzake wanajua cha kufanya, mifano tunayo kwa sababu kabla ya hapo ameanza kuuza viwanja kadhaa vya serikali bila kuishirikisha CHS na alipoona mkurugenzi wa CHS anafatilia na kuulizia, alimsimamisha kazi akavunja bodi ili yeye aendelee kufanya mambo yake vizuri, muheshimiwa naibu spika inasikitisha sana kwa sababu tunabodi kadhaa tunaonyesha kabisa na kwa ushahidi kwamba hapa kuna shida lakini hawavunji ikiwemo bodi ya pamba, tumeshasema mara kadhaa msifanye maamuzi kwa maslahi yenu binafsi, vunjeni bodi hii undeni nyingine…. hamvunji! tunajua kabisa kwamba ulinzi huu mnaowapa sio bure”

Kwa kumalizia, Filikunjombe amesema “kwenye maslahi yenu binafsi mnavunja na mnahakikisha kwamba mnaweza hata mkalidanganya bunge, mali za watanzania zinapotea nyie mnalindana, hapa tunasingizia sana watendaji wa chini kwenye halmashauri lakini mawaziri wetu wenyewe ndio wamegeuka kuwa mchwa, baadhi ya mawaziri wanatafuna nchi yetu mchana, muheshimiwa waziri mkuu hatuna imani na baadhi ya mawaziri wako”

No comments: