Monday, April 16, 2012

MELI YA MAGUFULI "TAWALIQ 1" YAANZA KUZAMA

ILE meli maarufu kama Meli ya Magufuli ambayo Serikali ya Tanzania iiliansa katika Eneo lake la bahari ya Hindi ikivua samaki bila ya kibali imenza kuzama baharini na imeharibika vibaya.
Inaelezwa kuwa Meli hiyo ya Tawaliq 1 Machi 8, 2009 ilikamatwa ikiwa na tani 293 za samaki aina ya Jodari iliyowavua katika bahari ya Hindi ndani ya Ukanda wa Kiuchumi wa Tanzania (EEZ), bila kuwa na kibali.
Meli ya Tawaliq 1 ilikamatwa ikiwa na wavuvi 34 na hadi kufikia tamati ya kesi hiyo jumla ya wavuvi 20 walitiwa hatiani.
Lakini licha ya Mahakama kuamuru meli hiyo itaifishwe kwa sababu ilikuwa haijulikani na tume inayojihusisha na shughuli za uvuvi katika Bahari ya India (IOCT) lakini meli hiyo imeanza kuzama kama inavyoonekana pichani.
Kuzama kwa meli hiyo ni kutokana na kutoboka baadhi ya maeneo hivyo kuingiza maji ndani.

No comments: