Monday, May 14, 2012

MAGARI MANNE YATEKETEA KWA MOTO MOROGORO


Moja ya mabasi yaliyoungua.
Wananchi waliofika eneo la tukio wakiyatazama magari yaliyoungua.
Mabasi madogo yaliyoungua na kubaki vyuma chakavu.
                                                         Umati uliofurika eneo la tukio.


MAGARI manne – mabasi madogo matatu na lori moja aina ya Fusso – yameteketea kwa moto katika maeneo ya kulazia magari ilipo ofisi ya Ofisa Mtendaji wa Kata ya Kihonda mkoani Morogoro.

Wenye magari ambao huyalipia sh. 1,000 kwa gari kubwa n ash. 500 kwa gari dogo, walishangaa kuyakuta magari yao yakiwa yameteketea kwa moto na kubaki vyuma mtupu.

Inaaminika kwamba moto ulioyaunguza ulisababishwa na wizi wa mafuta kutoka katika mgari yanayoegeshwa hapo, wizi ambao hufanya na vijana kwa kushirikiana na walinzi.

Hata hivyo, mmoja wa walinzi wa ofisi hiyo, John Pyuza Madala, alipohojiwa na mtandao huu, alikanusha madai hayo akisema moto huo ulitokana na shoti ya umeme.

Naye Ofisa Mtendaji wa kata hiyo, Hellena Mgala, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na akasema mmoja wa walinzi wa ofisi hiyo, Msafiri Said, ana kesi mahakamani inayohusiana na wizi wa mafuta kutoka katika magari yanayolazwa hapo.

 

No comments: