Wednesday, June 20, 2012

Mdau alia na uvunjifu wa sheria jijini arusha



Na Mahmoud Ahmad, Arusha
Kwa hili lazima tulikemee la kuvunja sheria za nchi na halmashauri kwa baadhi ya wanasiasa kuwaambia watu kutolipa fedha za taka na kutohama sehemu za kingo za barabara na mabarazani mwa maduka sanjari na nje ya masoko yetu wanakofanyabiashara jijini Arusha. https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiYy1HI-PVJ4GzHoVIJnsmiExzD58ILOoF4jphEzyOlUVJTUjn3rPLGlWrNtx5oeOauyskWWqjquY0fAC5B1Kip_LIfqu_BwbT1OA-Bfx4eDYo-Hv_rsMUR03YluuE83VBr4XKHkd6U_08/s1600/IMG_6617+-+Copy.jpgKumekuwa na wimbi kubwa la uvunjaji wa sheria na kila halmashauri ikiwataka kuhamia kwenye masoko yaliyojengwa kwa nguvu zetu sisi wenyewe hukataa kwa madai kuwa kuna mwanasiasa amewaambia waonyeshwe kwanza pakwenda wakati teyari halmashauri imeshawambia mahali pa kwenda huku ni kuvunja sheria tulizojiwekea. Jiji la Arusha lenye sifa ya kuwa jiji la utalii limekuwa dampo sasa kwa kila anayetaka kufanyabiashara kufanya biashara sehemu yeyote mradi apate maslahi yake. Ukipita soko kuu la jijihttps://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgndwyikPqff13g4SQB6a-3kfTP0YZVkbhH6IwnP_1bcsWSD-ENWYSlmDzi-9l4Inde4W-fqvd4yFihLPi1tdISTq-AWCdQ4VbUO-BIjxAacm8sCOVOEgRP8WaruFzFrktQ8X0I-yPxwHQ/s1600/IMG_6903+-+Copy.JPG hili utajionea biashara zinafanya hadi kwenye kingo za barabara na kila halmashauri inapotaka kuwaondoa wamekuwa wanapigana na mgambo na wengine kubeba mapanga huku ndiko tulikofikishwa na wanasiasa wa majitaka.Tufike mahali tukemee kwa nguvu zetu hali hii kwani inataka kulifanya jiji letu kuondokana na sifa ya kuwa jiji la mfano hapa Afrika ya mashariki kwa kuliundia sheria ndogo ndogo ambazo teyari mwanasheria wetu wa halmashauri ameziainisha kwa ajili ya mchakato wa maoni yanayoendelea kutolewa. https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiuPf3gP9qrGh6e7-hRgaxL_FZAm3mDfbEIUxMYCvBD2VXUJAy0zaTYkuDZ4vLoFPIK7jE79tgpvBOdqbhKeNrAgr8xIwy7KIbFbAB6I2Hfg_SPoN-u0VRCnYpFwM8I6J4Tn3OpUZ1NTnY/s1600/1+-+Copy.jpgWananchi wasiwe wakwanza kuvunja sheria na kuwaogopesha viongozi kusimamia sheria za nchi kwa kutaka maslahi yao ilimradi wamevunja sheria nasi tukabaki kuwaangalia bila ya kutimiza majukumu yetu kwa mujibu wa sheria za halmashauri. Kumekuwa na ujenzi holela unaofumbiwa macho na wakuu wa idara za halmashauri yetu kiasi kuwa jiji hili limekuwa na ujenzi wa makazi ya watu kwa kasi ya ajabu kuliko majiji yote hapa nchini bila kufuata mipango miji nasi kuendelea kukaa kimya na sheria zinavunjwa na wachache kwa maslahi yao binafsi. https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhBfzrC-VxKKe7ioVcvV61MG5n_Fn5hRdGJEt2_9fvOiFj9KDEp1eHpQcMGAtrJB_Hxq_0eWZ7axb32pDNJmMzID3QjaNgexr92gAYanNYfE8NGIzX_8BkJAIYlXv-9CRiP079gsLqu_2k/s1600/6+-+Copy.jpgWimbi la upandishaji tozo ya majengo kiholela nayo ni moja ya mambo ambayo yamekuwa ni kitanzi kwa wananchi na kuwatakiwa mwanasheria kubuni njia mbadala ya kuwafanya watu kulipa tozo hizo za sasa kabla hawajapandisha tozo nyingine kwani wameshindwa kuonyesha hata data base ya halmashauri hii nayo ni uvunjaji wa sheria zetu tulizojiwekea. Ukusanyaji wa tozo hapa ni tatizo siyo kuongeza tozo tufike mahali tuangalie makusanyo yetu yanakidhi vigezo tulivyojiwekea au la ndipo mwanasheria atuambie suala zima la kuongeza kodi ya majengo. https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEh-LQ4VjSDlD5GI6ueicSLUCoguysxoZuA4iPoxjEcJ4qjBJyNUwaEjxc9xPyLSoxLD9UfMi14bPhYM_akRhAx_-5_OGMY1pMVSDU9DvaNxRqs5S3ETyuB1slBflI92WCl0huMuJXBxrbM/s1600/8+-+Copy.JPGWananchi na viongozi wetu tukae na kujadili wapi tunapoelekea badala ya kutafutana uchawi huku tunaendelea kuvunja sheria na kuundiana sheria kwa kukomoana bila ya kuangalia vipato vya wananchi na kushindwa kukusanya mapato ya halmashauri isiwe ndiyo kigezo tukusanye kwanza tuone halafu kama kuna upungufu ndipo tuweze kuongeza tozo. Wakazi wa jiji hili hasa wafanyabiashara tuwe macho na kuacha kuvunja sheria za nchi kwa kukataa kutii sheria za kuhama kwenda kwenye masoko mapya je hatujali fedha zetu tunazo tozwa na halmashauri tusiwe wa kwanza kuvunja sheria za nchi kwa maslahi binafsi ya wanasiasa.

No comments: