Wednesday, June 20, 2012

SEHEMU ZA SIRI AKIKWEPA UKIMWI
Na Shomari Binda
Musoma.

Mwanaume mmoja mkazi wa Buhare katika Manispaa ya Musoma amefanya maamuzi magumu ya kujitoboa na mdenge katika sehemu zake za siri na kufunga kufuli kwa kile alichokieleza kujilinda na kuzuia kupata maambikizi ya virusi vya ukimwi.

Akiongea mbele ya Waandishi wa Habari wakiwa katika maazimisho ya siku ya mtoto wa afrika mwanaume huyo ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini licha kukubali kupigwa picha alisema ameamua kutoboa sehemu hiyo na kufunga kufuli kutokana na kufanya vitendo vya ngono isiyo salama kwa muda mrefu akiwa katika masuala ya uvuvi na kujua moja kwa moja amekwisha upata ugonjwa wa ukimwi.

"Ndugu Waandishi kwa kweli nimefanya mambo machafu kwa muda mrefu sana na niliugua kiasi cha ndugu kunikataa na kujua tayari nimekwisha kuathirika lakini nilipimwa zaidi ya mara nne nakugundulika sina virusi vya ukimwi na ndio nimeamua kufanya maamuzi haya magumu lakini sitaki wengine wafanye kama ambavyo nimefanya,"alisema mwanaume huyo.


Alisema uamuzi huo aliochukua tangu Mwaka 2009 umemsaidia kupunguza vitendo vya ngono alivyokuwa akivifanya na kuongeza kuwa licha ya kupoteza wazazi wake wawili yeye ndio anayewahudumia wadogo zake saba kwa kuwalipia karo za shule pamoja na mahitaji mbalimbali ya kifamilia ya kila siku.


Aliwaeleza Waandishi wa Habari kuwa ataendelea kuwa katika hali hiyo hadi pale atakapopata mwanamke mwaminifu atakayekuwa tayari kupima na kuonekana kuwa hana virusi vya ukimwi ndie atakaye ishi nae kama mume na mke katika maisha yake.


Aidha Mwanaume huyo ametoa wito kwa jamii hasa wanaojishughulisha na shughuli za uvuvi kuwa makini na kujihusisha na masuala ya ngono zembe na wale wenye wenza wao kuwa waaminifu kutokana na vitendo vya ngono kukithiri katika makambi ya wavuvi na kushindwa kujipatia maendeleo.


Mwaka 2005 Mwalimu mmoja aliyekuwa akifundisha shule ya msingi Nyichoka Wilayani Serengeti alijikata sehemu yake ya siri na kuiondoa akidai hataki kupata maambukizi ya virusi vya ukimwi kutokana na kuandamwa na wanawake kila anapopata mshahara mwisho wa mwezi.

No comments: