Thursday, June 21, 2012

SEMINA YA KUELEKEZA UMMA JUU YA MABADILIKO YA MFUMO WA UTANGAZAJI ARUSHA



Mkuu wa wilaya ya Arumeru Mhe. Nyerembe Munasa akiwasisitiza wadau hao kuwaeleza wananchi wao juu ya kupokea mabadiliko hayo ambapo wanapaswa kufanya maandalizi mapema ya kuhama katika mfumo wa analojia kwenda digitali. Kushoto ni Mkurugenzi wa Mawasiliano TCRA Bw Habbie Gunze na kulia ni afisa wa TCRA


Wadau wa sekta ya mamlaka ya mawasiliano tanzania(TCRA) wakiwa wanasikiliza kwa makini maelekezo kuhusu mfumoCwa mabadiliko ya anaelojia ya utangazaji kwenda digitali unatarajiwa kuanza kutumika rasmi Januari 2013. Picha zote na Mary Ayo. Mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) ipo katika kuutangaza mpango kazi wa kuandaa wananchi kuingia kwenye teknolojia mpya ya utangazaji wa digitali katika mkutano wake wa kutimiza miaka kumi kwa utangazaji nchini.

Mkurugenzi wa Mawasiliano wa TCRA, Bw.Habbie Gunze alisema kila mabadiliko ya teknolojia yana gharama zake, na kuwa katika mabadiliko hayo kuna watu ambao watalazimika kubadili televisheni zao na wengine kununua ving'amuzi.

Alisema mfumo wa digital umechangia kukua kwa haraka na kubadili sekta ya utangazaji nchini ambako kumeleta muonekano mpya.Pia alisema kuingia kwa mfumo wa kasi wa intaneti katika Afrika Mashariki baada ya kuwepo mikongo miwili ya mawasiliano, Easy Fibre na Seacom, kumeongeza mawasiliano na matumizi ya teknolojia ya habari na mawasiliano nchini Tanzania.

Alisema mfumo huo utasaidia huduma nyingi za utangazaji na kutoa fursa mpya za kutengeneza vipindi kwa ajili ya mfumo wa utangazaji wa digitali.



No comments: