Monday, July 23, 2012

DIDIER DROGBA AANZA KUCHEZA CHINA, HIKI NDIO ALICHOFANYA KWENYE MECHI YAKE YA KWANZA!

Hamu ya kumuona Didier Drogba akicheza kwa mara ya kwanza toka aihame Chelsea na kwenda China imetimia, hiyo hapo chini ni video ikionyesha kazi aliyoifanya Didier Drogba muda mfupi tu baada ya kuingia akitokea benchi kipindi cha pili.
Timu yake ya Shanghai ilikua imeshafungwa moja tayari lakini alipoingia Drogba alisaidia na hatimae Cao Yunding kufunga goli la kusawazisha ambapo kabla ya hapo pia, Drogba alikosakosa magoli kadhaa likiwemo la kichwa na moja baada ya kuachia mkwaju ambao ulipanguliwa kwa tabu na kipa wa Guangzhou .
Hii ni mechi ya kwanza ya Drogba toka ajiunge na club hiyo ya China kwa dili la miaka miwili akiwa na mchezaji mwenzake wa zamani wa Chelsea Nicolas Anelka…. chek jinsi Drogba alivyocheza kwenye hiyo mechi yake ya kwanza ndani ya hiyo video hapo chini…..
.

No comments: