Saturday, July 28, 2012

SHIGONGO, KINYONGA NA NABII FEKI


Mkurugenzi wa Global Publishers, Eric Shigongo(kati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya msanii huyo na kushoto ni Meneja Mkuu wa Global Publishers, Abdallah Mrisho.
Baadhi ya wanahabari wa vyombo mbalimbali vya habari wakimsikiliza kwa makini Eric Shigongo.
JD akisisitiza jambo (kulia) Juma Mbizo, Mratibu wa Matamasha.
Eric Shigongo (kulia) akisikiliza maswali kutoka kwa waandishi wa habari.
MD wa Global Publishers Ltd, Eric Shigongo, mapema leo ameongea na media kuhusu madai ya Jose Chameleone kudai paspoti yake, ambaye jana alikwenda Ubalozi wa Tanzania nchini kwake Uganda kushinikiza kurejeshewa paspoti yake.
Eric amefunguka kwa kusema kuwa, kampuni yake na msanii huyo waliingia makubaliano ya kufanya shoo kwenye Tamasha la Usiku wa Matumaini, liliofanyika Uwanja wa Taifa Julai 7 mwaka huu, ambapo katika mazungumzo ya awali, msanii huyo aliomba kulipwa dola 5000 na kulipiwa tiketi 2 za ndege ili kuhudhuria tamasha hilo, masharti ambayo yalikubaliwa.
 Mazungumzo hayo ya awali yalifanyika kati ya Global Publishers na agenti wa Chameleone ajuliikanae kwa jina la George. Kabla ya kutuma fedha hizo, kampuni yake ilihitaji kujiridhisha kama ajenti huyo alikuwa kweli anawasilina na kukubaliana na Chameleone kuhusu shoo ya Dar, ili kuepuka utapeli.
 “Tulipokubaliana nae kupitia ajenti wake, tuliamua kwenda mbele zaidi ili kujiridhisha, ambapo tuliwasiliana na mwanamuziki Kidumu ambaye anamfahamu huyo George na kwenda mpaka Kampala kukutana ana kwa ana na wahusika, kwa niaba yetu”, alisema Shigongo.
 Akielezea zaidi, Shigongo alisema kuwa Kidumu alikwenda Kampala na kukutana na George pamoja na Jose Chameleone, ambaye alikubali kuja kufanya shoo na kumruhusu Kidumu kusainishana mkataba na ajenti wake na kumpatia hizo fedha.
 “Chameleone alitoa ruhusa kwa ajenti wake kusaini mkataba na kupokea advace ya dola 3,500 kwa niaba yake kwa madai kuwa yeye asingeweza kusubiri malipo wakati huo kwa sababu alikuwa anawahi sehemu nyingine.
 “Baadae Jose alikuja kugeuka na kudai hakupewa hizo pesa na ajenti wake, kitu ambacho kilonekana kama mchezo wa kitapeli kati ya Chameleone na ajenti wake kwetu sisi.
 “Kwa kuwa ujio wake Tanzania ulikuwa umeshatangazwa sana, uongozi wa Global Publishers, ulilazimika kufanya mazungumzo mengine na Chameleone na kumuomba sana kuja nchini kufanya shoo, ambapo this time akakubali kwa masharti ya kulipwa dola 8000 na tiketi nne za ndege.
“Ndugu zangu, sikua na jinsi, nililazimika kumkubalia na kumlipa dola 8000, kwa sababu tayari tamasha lilikuwa limeshatangazwa sana, billboards zimewekwa barabarani na promosheni kubwa ilikuwa inafanyika,” alisema Shigongo kwa uchungu.
Hivyo mara baada ya kukubaliana, safari hii akalazimika kumtuma meneja wake kwenda mpaka Kampala na kukutana na Chameleone ana kwa ana na kumpatia dola 8000 na kusaini mkataba mwingine wa pili.
“Ni dhahairi kabisa alichokifanya Chameleone kilikuwa ni utapeli kwa kushirikiana na ajenti wake, kwa sababu tunamuamini Kidumu ambaye tumeshafanya naye kazi mara Kadhaa kwa uaminifu mkubwa. Pia ni Chameleone ndiye aliyemuidhinisha ajenti wake kuchukua pesa hizo, hivyo ulikuwa ni mchezo wa pamoja,  na hiyo ni tabia ya Chameleone, kwani ameshawafanyia mapromota wengi kiasi kwamba hivi sasa hakanyagi nchini Kenya.
 “Dola 3,500 siyo fedha nyingi, ningeweza kuzisamehe, lakini nimeamua kuzidai kwa manufaa ya watu wengine, Watanzania tusikubali kufanywa wajinga kwa sababu ya upole wetu, tutaendelea kudhauriwa na kufanywa wajinga mpaka lini,” alihoji Shigongo.
Mwisho Shigongo alitoa wito kwa Watanzania kuungana katika suala hili, kwani Chameleone ameonesha dharau kubwa kwa Watanzania kwa kumfuata balozi wetu nchini Uganda na kuondoka ofisi kwake huku akisonya na kubamiza mlango, akiendelea kuonesha dharau kwa Watanzania wote wapatao miloni 40!

Mke wa tatu
Stori: Issa Mnally na Richard Bukos
NABII aliyesemekana ni wa Kanisa la Mashahidi wa Yehova la Kibamba, jijini Dar, Joseph Buberwa ameingia kwenye skendo ya kudaiwa kutelekeza wake zake wawili na watoto, sasa ameshatoa mahari na yupo mbioni kufunga ndoa na mwanamke mwingine wa tatu aitwaye Sarah (18).

Mke wa pili
Kwa mujibu…

Mke wa tatu
Stori: Issa Mnally na Richard Bukos
NABII aliyesemekana ni wa Kanisa la Mashahidi wa Yehova la Kibamba, jijini Dar, Joseph Buberwa ameingia kwenye skendo ya kudaiwa kutelekeza wake zake wawili na watoto, sasa ameshatoa mahari na yupo mbioni kufunga ndoa na mwanamke mwingine wa tatu aitwaye Sarah (18).

Mke wa pili
Kwa mujibu wa chanzo makini, uamuzi wa nabii huyo unatokana na madai yake kwamba alioteshwa na Mungu kuwapiga chini wake zake hao kwa vipindi viwili tofauti kutokana na matatizo ambayo yangemtokea mbele endapo asingewaacha.
Chanzo hicho kilisema vitendo vya nabii huyo anayeonekana kwenye televisheni moja nchini akitoa neno la Mungu, vimekuwa vikichafua sifa ya unabii wake bila mwenyewe kujua.
Jirani huyo ambaye jina lake tunalihifadhi, alisema awali, nabii huyo alimpiga chini mkewe wa kwanza aitwaye Dina ambaye alibahatika kuzaa naye mtoto mmoja.

Mke wa kwanza
Baada ya kumtosa Dina alimpata mwanamke mwingine aitwaye Riziki ambaye naye alizaa naye watoto wawili lakini baada ya muda na yeye akamuona hafai na kuopoa kifaa cha sasa, Sarah.
Baada ya taarifa hizo, mapaparazi wetu walianza kuutafuta ukweli ambapo walimnasa Riziki kwa njia ya simu.
Mwanamke huyo alikiri kutokea kwa yote hayo ambapo alisema kabla ya kugundua kuwa mumewe amepata mwanamke mwingine alianza tabia ya kulala nje ambapo baadhi ya majirani walimwambia huwa wanamuona na msichana.


Watoto
“Baada ya majirani kunitonya kuwa amepata mpenzi mwingine ambaye amekuwa akionekana akitanua naye sehemu mbalimbali niliwavizia, ndipo siku moja nikiwa na kundi la majirani tulimfuma na Sarah pale Mlimani City,” alisema Riziki.
Akaendelea: “Katika fumanizi hilo, uzalendo ulinishinda hivyo niliwavaa na kutaka kuwafanyia varangati lakini majirani nilioongozana nao walinikamata ndipo wao wakapata upenyo wa kukimbia.”
Kwa mujibu wa uchunguzi, Riziki akiwa kwenye harakati za kumrudisha nyumbani mumewe, Jumapili iliyopita, Nabii Buberwa alikwenda kutoa mahari nyumbani kwa akina Sarah na kuangusha bonge la pati na pombe za kumwaga.
Mapaparazi wetu walimtafuta nabii huyo ambapo alipopatikana alikiri kuwahi kuwa mume wa Dina na kuzaa naye mtoto mmoja kisha kumtosa na kuishi na Riziki ambaye alizaa naye watoto wawili na kumtosa na sasa ameshatoa mahari kwa akina Sarah.
“Ni kweli ndugu waandishi, niliwahi kuishi nao wote hao lakini kwa mujibu wa maono niliyopewa na Mungu, Sarah ndiye mke wangu nitakayefanikiwa katika maisha hivyo Jumapili nilishatoa mahari na hivi karibuni tutafunga ndoa.
Jitihada za kumpata Dina ziligonga mwamba. Aidha, Risasi Jumamosi lilipowasiliana na Kanisa la Mashahidi wa Yehova Makao Makuu, jijini Dar walisema Nabii Buberwa alishawekwa kando na kanisa hilo lakini wamekuwa wakisikia bado anatumia jina lao.


No comments: