Katika harakati za kuimarisha zoezi la ukataji tiketi za treni ya abiria Menejimenti ya Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) imetoa Mwongozo ufuatao: TUNAPENDA KUWAFAHAMISHA WATEJA WETU KWAMBA, KUANZIA JUMATATU JULAI 16, 2012 MTEJA YEYOTE ANAYETAKA KUNUNUA TIKETI YA TRENI LAZIMA AONESHE KITAMBULISHO CHAKE KWA KARANI MUUZA TIKETI BILA HIVYO HATUTAWEZA KUMHUDUMIA. VITAMBULISHO VINAVYOTAMBULIKA NI VIFUATAVYO; KITAMBULISHO CHA KUPIGIA KURA, LESENI MPYA YA UDEREVA, KITAMBULISHO CHA MUAJIRI, HATI YA KUSAFIRIA, KITAMBULISHO CHA SHULE, BARUA KUITOKA KWA MWENYEKITI WA SERIKALI YA MITAA NAKADHALIKA UTARATIBU HUU MPYA NI KWA AJILI YA KUONGEZA UFANISI NA KUBORESHA HUDUMA ZETU KWA WATEJA WETU! IMETOLEWA NA MENEJA UHUSIANO ( MIDLADJY MAEZ) KWA NIABA YA KAIMU MKURUGENZI MTENDAJI WA TRL MHANDISI KIPALLO AMAN KISAMFU DAR ES SALAAMJULAI 16, 2012 |
This blog is for critical thinkers, people with open mind, ready to accept criticisms and work on them. Sharing the know-how, skills and experiences of Life and Technology at large. You are warmly welcome!! ---------------------------------------------------- Blogu hii ni kwa ajili ya wenye fikra makini wapendao kupokea na kufanyia kazi ukosoaji. Walio na mtazamo chanya tena mpana katika kushirikishana maarifa, ujuzi na uzoefu wa maisha na teknolojia kwa ujumla wake. Karibuni sana !!!
Tuesday, July 17, 2012
UTARATIBU MPYA WA KUKATA TIKETI-TRL
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment