Friday, September 28, 2012

MUONEKANO MPYA WA TBC 1

Sasa TBC 1 wameanza kutumia "Watafsiri wa lugha za Alama kwa wasiosikia" katika taarifa zao za habari kama anavyoonekana huyo dada kulia kwa picha hii. Pia muonekano umebadilika, Angalia neno "LIVE" sasa lipo chini kushoto na chini yake kuna tarehe ya siku hio. Utepe wenye neno "HABARI" nao umebedilishwa aina ya mwandiko (Font), ya sasa inapendeza zaidi kwa kweli. Tazama taswira zinazofuata utaamini nikwambiayo.


Katika kila picha nilikua nafuatilia huyo mtafsiri wa lugha ya alama alivyokuwa akifanya, nikaamini ni Elimu inayojitegemea, lazima ufundishwe kubahatisha utasababisha usieleweke kwa wasisikiaNo comments: