Wednesday, October 3, 2012

TRL yaelezea mchakato wake wa kuanzisha usafiri wa treni jijini Dar

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhrFwqEhi0-UfjQTLp_KPe0o-Jv_JsTVQ3PZ4FP91n0UBfhBnMRLweW1XREOZSBZkL2WhgjmAQqhvdzz0G3Vwlir4mKJw-o8QqzpT5-Lo3xtEWUJslw9rLSJ3Li6K9Xj_ZuHZeYw772rEU/s1600/treni+majaribio+dar+-1.JPG


Uongozi wa
Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) unapenda kuwataarifu Wateja na  Wananchi wa Dar es Salaam
kwa ujumla kuwa taarifa iliyotolewa na Gazeti la kila siku la Mwananchi toleo
la siku ya Jumanne Oktoba 02, 2012 kwamba SUMATRA
ndiyo kikwazo cha kuanza kwa huduma ya usafiri wa treni jijini Dar es Salaam
siyo sahihi.


https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEg3lodhiANXFRh9u9L-qy5X8unyGnBWYvEkYbxeuEH6J4HGjps5PBJZdlu_3yg9xH2L_ag6XGmimfxclUVtjvG5D69Y_hoE_AyI6aO1PBpeLhxvpTWfwYfxgP3uE6bJ_Mz89yp8bAydo9c/s1600/treni+majaribio+dar+-+6.JPG
 
Katika mchakato
wa kutoa  huduma za usafiri wa treni
ambayo hapo awali haikuwepo jijini, wadau wa kufanikisha mradi huu  ni taasisi nyingi ambazo zinapaswa kuchangia
kuanzishwa kwake. Hivyo basi mchakato huo ni wa lazima na
hakuna njia ya mkato . Tunapenda kueleza wazi kuwa  siyo sahihi kusema kuwa TRL imekwama kuanza
kutoa huduma ya usafiri wa treni ya 
abiria jijini kutokana na SUMATRA kutoidhinisha viwango vya nauli na
kutopewa leseni. https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiI5KdaaI-asIxv5Ffz5To5bd1lMS7egF37CW5Zj_JT3roVHTx9gWCcr5eUaVVDqZC2Zp040po5lov4a2woMHpdH53H5rUeLOjstmQIpQKZocPY4sKlrqxNsvVIT4Dk1dtrcm2gws_BYq0/s1600/treni+majaribio+dar+-+5.JPG

Uongozi
wa TRL unapenda kutoa rai kwa Waandishi habari na Wahariri wao kabla ya
kuchapishwa habari nyeti kama hii inayogusa maslahi ya Wadau wengi na hasa wale
wanaongojea kwa hamu huduma hii ianze kujitosheleza  kuwa habari wanayoichapisha ni sahihi na kama
inajenga au kubomoa.

 
Ukweli ni kwamba TRL hivi sasa inakamilisha
mchakato wa kuandaa na  kuwasilisha
vigezo ambavyo vinahitajika na SUMATRA ili
iweze kufanya tathmini yake na hatimaye kutoa leseni ya huduma ya treni jijini

Tunarudia Uongozi
wa TRL unasikitika kwa usumbufu uliotokana na taarifa hizo zisizo sahihi kwa
Wadau wote na hasa kwa  Uongozi wa SUMATRA.

Imetolewa na Afisi ya Uhusiano kwa

Niaba ya  Kaimu Mkurugenzi
Mtendaji wa TRL

Mhandisi Kipallo A. Kisamfu

Dar es salaam,

Oktoba 2, 2012

No comments: