Sharo
Milionea aliponaswa na mtandao huu wakati akifanya shopping mwezi huu
katika duka la Robby One lililopo Kinondoni jijini Dar ambapo alisema
ili uwe sharobaro wa ukweli inabidi usiwe mbahili katika kununua nguo
kila mara ili uendane na staili hiyo ya usharobaro.
KOMEDIAN ambaye pia alikuwa
msanii wa muziki wa Bongofleva, Hussein Mkieti ‘Sharo Milionea’
amefariki dunia leo majira ya saa mbili usiku katika ajali ya gari.
Sharo amefikwa na mauti wakati akiwa safarini akitokea Dar es Salaam
kuelekea nyumbani kwao, Kijiji cha Lusanga, Muheza mkoani Tanga. Msanii
huyo alikuwa anaendesha gari aina ya Toyota Harrier lenye namba za
usajili T478 BVR na amepata ajali eneo la Songa- Maguzoni wilaya ya
Muheza mkoani Tanga. Marehemu alikuwa peke yake kwenye gari. Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Tanga, Costantine Massawe amethibitisha kutokea ajali
hiyo na katika
taarifa yake kwa vyombo vya habari saa chache baada ya ajali, alisema
kuwa mchoro wa ajali unaonesha kuwa gari la marehemu liliacha njia kabla
ya kupinduka mara kadhaa. Naye Mkuu
wa Wilaya ya Muheza, Subira Mgalu amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo
na kubainisha kwamba gari alilopata nalo ajali limeharibika sana.
“Mimi sijafika eneo la tukio
lakini nimezungumza na OCD wetu hapa Muheza, Andrew Satta yeye alifika
eneo la tukio na kunipa taarifa kamili. Ukweli ni kwamba msiba huu ni
majonzi na pigo kubwa kwa Wilaya ya Muheza kwa sababu huyu kijana ni
mzawa wa hapa.
“Muheza tulikuwa tunajivunia
kipaji cha Sharo Milionea lakini hatuna jinsi, kila kitu kinapangwa na
Mwenyezi Mungu,” alisema Mgalu.
No comments:
Post a Comment