Mchezaji Christopher Katongo ameshinda tuzo ya mwanasoka bora wa BBC kwa mwaka 2012.
Nahodha huyo wa Zambia mwenye umri wa miaka 30 amemshinda Demba Ba, Didier Drogba, Younes Belhanda na Yahya Toure na kuwa mshindi wa kwanza kutoka Kusini mwa Afrika katika historia ya mashindano hayo.
Orodha ya washindani hao ilitangazwa na wataalamu wa soka Afrika, ambao wamezingatia umahiri wa mchezaji, uwezo wa kiufundi na ushirikiano na wachezaji wengine.
Idadi kubwa ya watu wamepiga kura kupitia njia ya mtandao au ujumbe mfupi huku asilimia 40 kati yao wakimchagua Katongo, ambaye anachezea timu ya China Henan Construction.
No comments:
Post a Comment