NDEGE YA TANAPA YAANGUKA RUBANI ANUSURIKA KIFO
Ndege
yashirika la hifadhi la taifa (TANAPA) yenye namba za usajili 5H-PZS
aina ya C182 ikiwa imeanguka katika eneo la nsemulwa mjini Mpanda muda
mfupi baada ya kuondoka katika uwanja wa ndege wa mjini mpanda ikiwa
inaendeshwa na rubani Adam kajwa aliepata majeraha sehemu ya uso. Ajali
hiyo imetokea majira ya saa 10:55 jioni wakati ndege hiyo ikielekea
hifadhi ya taifa ya katavi wilayani mlele mkoa wa katavi. Picha na Walter Mguluchuma
*****
Ndege ya hifadhi
ya taifa ya TANAPA imepata ajari ya kuanguka
wilayani Mpanda mkoa wa Katavi
na rubani wa ndege hiyo
kunusurika kifo baada ya kupata majeruhi
Meneja wa uwanja
wa ndege wa Mpanda Mahamud Muhamed alisema
ajari hiyo ilitokea jana
majila ya saa 10 na dakika 55 jioni katika
kijiji cha Nsemlwa wilayani hapo
ndege hiyo iliyo
anguka ilikuwa namba za
usajiri 5H-- FZS aina
ya C182 ndege ndogo ya abiria
mari ya hifadhi ya taifa ya
TANAPA iliyo kuwa ikiendeshwa na
rubani Adamu Athumani
Kajwaa yenye uwezo wa kuchukua
abiria wane
Muhamed alieleza kuwa
ndege hiyo ilikuwa imetoka katika uwanja wa ndege wa mpanda ikielekea
katika hifadhi ya wanyama pori ya
Katavi wilayani Mlele
Ajari
hiyo ilitokea umbali wa
kilimeta moja na nusu
kutoka uwanja wa ndege wa Mpanda
mara baada ya
kuondoka katika uwanja huo ambapo
imeharibika sana sehemu ya bawa lake na upande wa injini.
Meneja wa uwanja huo wa ndege alisema
taarifa za awali
zinaonyesha chanzo cha ajari
hiyo kilitokana na njini
ya ndege hiyo kufeli wakati ikiwa angani
Rubani wa ndege
hiyo alipata msaada wa wa
kuokokewa na wananchi waliokuwa
wakifanya shughuli za
kilimo kwenye mashamba
yao
Mmoja wa
walio shuhudi tukio hilo Credo Mwanisenga alieleza
kuwa wakati akiwa
anafanya shughuli zake za kilimo
ghafla aliona ndege
iliyo kuwa angani
ikizimika na kisha baada ya
muda mfupi ikaanguka
jirani na mti wa mwembe
Na mara walifika katika eneo hilo kwa lengo la kutowa msaada hata hivyo
iliwachukuwa muda kuanza kutowa
msaada kwa rubani huyo
aliye kuwa ndani ya ndege peke
yake kutokana na eneo hilo kuwa na nyuki wengi ambao walianza kuwashambulia waokoaji hao
Hata hivyo waliewza
kufanikiwa kumtoa rubani huyo
huku akiwa amepata majeruhi makubwa sehemu ya uso
wake na maumivu sehemu ya kifua huku akiwa anakohoa damu na aliewza
kukimbizwa haraka katika hosptali ya
wilaya ya mpanda baada ya kupata msaada
wa gari la meneja wa uwanja wa ndege aliye fika kwenye eneo la tukio
Rubani wa ndege hiyo aliweza kupatiwa matibabu katika hospitali ya wilaya yam panda kwa kushonwa nyuzi nane katika
paji la uso wake na kasha aripewa
ruhusa.
No comments:
Post a Comment