Sunday, January 6, 2013

MTOTO MIAKA 16 ASHIRIKI MASHINDANO YA PIKIPIKI, ALIA BAADA YA KUSHINDWA

Ally Ramadhani 'Dogo Ally' akimtimulia vumbi mpinzani wake Theo John (hayupo pichani) wakati wa mashindano.
Dogo Ally akiwa amemtangulia Theo kabla pikipiki yake haijaharibika.…
Ally Ramadhani 'Dogo Ally' akimtimulia vumbi mpinzani wake Theo John (hayupo pichani) wakati wa mashindano.
Dogo Ally akiwa amemtangulia Theo kabla pikipiki yake haijaharibika.
Pikipiki ya Dogo Ally ikitolewa uwanjani baada ya kuharibika.
 
Dogo Ally akilia baada ya kushindwa kuendelea na mashindano.
Dogo Ally na Theo John kabla ya kuanza mashindano.
ALLY  RAMADHANI (16) aliyekuwa akishiriki mashindano ya pikipiki kwenye Uwanja wa Saba Saba mjini Morogoro aliangua kilio hadharani baada ya pikipiki yake kuharibika wakati akiongoza na hivyo kupitwa na mpinzani wake ambaye alishinda na kupewa zawadi.
Theo John (30) ndiye aliyetangazwa mshindi wa shindano hilo japokuwa mashabiki wa Ally walitaka shindano hilo lirudiwe lakini watayarishaji walikataa.
Pamoja na kilio cha Ally, mashindano hayo yaliingia dosari wakati mmoja wa washiriki aliyejulikana kwa jina la George alipoanguka na kusababisha taharuki kubwa uwanjani hapo.
(PICHA/HABARI: DUSTAN SHEKIDELE,  GPL / MOROGORO)

No comments: