Saturday, January 5, 2013

RAIS KIKWETE AONGOZA MAMIA KUMZIKA JUMA KILOWOKO 'SAJUKI' JIJINI DAR JANA

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka udongo katika kaburi la marehemu Sadick Juma Kilowoko 'Sajuki' leo.
Baba mzazi wa Sajuki, Mzee Kilowoko, akiweka udongo katika kaburi la mwanaye.
Mwili wa marehemu Sajuki ukishushwa kutoka kwenye gari.
...Ukipelekwa makaburini.
...Mwili wa marehemu Sajuki ukipelekwa makaburini kwa maziko.
Kaburi alipolazwa marehemu Sajuki.
Mwili wa Sajuki ukiteremshwa kaburini.
Mazishi ya Sajuki yakiendelea.
Rais Kikwete pamoja na Simon Mwakifwamba wakifuatilia mazishi ya Sajuki.
Umati wa watu waliohudhuria mazishi hayo.
---
MAMIA ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam leo wamejitokeza katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam kumpumzisha mpendwa wao, Sadick Juma Kilowoko 'Sajuki', aliyefariki dunia alfajiri ya Januari 2, mwaka huu (Jumatano) katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Miongoni mwa waliomzika Sajuki ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete.
(PICHA NA RICHARD BUKOS / GPL)

No comments: