Tuesday, January 15, 2013

Na Mwandishi Wetu
MWENYEKITI wa CCM, Tawi la Washington DC, Marekani, Loveness Mamuya, yupo kwenye uhasama mkali na Mtanzania mwenzake anayeishi nchini humo, Linda Bezuidenhout, kiasi cha kuchafuana na kuibua aibu nzito.
 
Linda Bezuidenhout.
Rekodi zinaonesha kuwa Loveness na Linda walikuwa marafiki wakubwa lakini kwa sasa ni maadui wasiopikika chungu kimoja, huku mitandao ya kijamii, hususan Facebook na skendo ya usagaji, vikitajatajwa katika malumbano yao.
Baada ya malumbano na kuchafuana, wiki iliyopita mwandishi wetu aliwapata mahasimu hao, akarekodi sauti zao ambapo kila mmoja alitoa ya moyoni kuhusu mwenzake.
ALICHOKISEMA LINDA
Linda ambaye ni dada wa mshindi wa Big Brother Africa mwaka 2007, Richard Bezuidenhout alidai: “Tatizo kubwa la Loveness ni usagaji. Miaka saba iliyopita wakati naishi Maryland (Marekani), nilikuwa na matatizo ya nyumba. Nilikuwa sina hati za kuniwezesha kupanga nyumba yangu mwenyewe.
“Nikawa nachangia nyumba na watu wa nchi nyingine, nanyanyasika, tunagombana. Loveness akasikia matatizo yangu, akanipigia simu. Akaniambia ananijua tangu nikiwa Dar es Salaam. Baadaye akanishawishi nihamie kwake halafu atanisaidia kupata hati niweze kupata nyumba niishi mwenyewe na watoto wangu. Wakati huo nilikuwa na watoto wawili, mmoja ana miaka sita, mwingine mmoja na nusu.
“Nilipohamia nyumbani kwake, siku zikawa zinakwenda hafuatilii makaratasi yangu wala hataki kujishughulisha kunitafutia nyumba. Kinyume chake akawa ananitongoza tusagane, mimi nikamkatalia, basi akawa ananifuata chumbani usiku, ananilazimisha tufanye huo mchezo wa kusagana.
“Kila siku alikuja chumbani kwangu, mimi nikawa nashindwa kumjibu kwa ukali kwa kuhofia atanifukuza, nikawa nasingizia watoto wangu hawajalala, yeye anasema wamelala, mimi naendelea kumsisitizia hawajalala kwa sababu mimi ndiye nawajua.
“Siku zikawa zinakwenda, siku moja nikamuuliza ni kwa nini hataki kunisaidia kupata nyumba, au mpaka anifanyie huo mchezo? Hapo nikawa nimemtibua lakini baadaye ikabidi nijifanye nimelainika, akatulia lakini nikaendelea kumkatalia kijanja kunifanyia huo mchezo wake.
“Kuna wakati alinunua mpaka nyeti bandia ya kiume akidhani mimi nitakubali. Vilevile kuna siku alinibaka, hiyo siku siku alinunua pombe tukalewa, nilipolala, katikati ya usingizi nikashtuka kusikia mtu amenilalia.
“Nikamsukuma, kutokana na pombe sikumzingatia, nikaendelea kulala. Asubuhi nikakumbuka lile tukio, nikamuuliza Loveness kama alikuja chumbani kwangu usiku, akanijibu ndiyo na nilimsukuma. Akaniambia pia kwamba hakutaka kuendelea kwa sababu aliponishika aligundua nilikuwa katika siku mbaya.
“Nikajua mambo yamekuwa mazito, kwa hiyo nikamuomba anisaidie kupata nyumba, baada ya hapo, atakuwa anakuja kwangu tunafanya huo mchezo kwa kujiachia. Kusikia hivyo, Loveness akaondoka na mume wake, wakaenda kutafuta nyumba, jioni wakaniambia wamepata.
“Yaani baada ya kumuahidi tutakuwa tunafanya mchezo wake ndiyo akapata nyumba haraka. Nikahamia na watoto wangu. Baada ya hapo, nikamhamishia na mdogo wangu mwingine. Loveness akaona mdogo wangu atakuwa anamfanya asifanikiwe lengo lake la kufanya mchezo wa usagaji na mimi.
“Loveness akanigombanisha na mdogo wangu, akahama lakini baadaye yule mdogo wangu akaja kunipa siri nzima ya maneno ya uchonganishi aliyokuwa anaambiwa na Loveness. Kwa kweli kitendo cha kunigombanisha na mdogo wangu kiliniudhi sana, ikabidi nianike uchafu wote na njama zake za kujidai ananisaidia ili anifanyie mchezo wa usagaji.”
 
Loveness Mamuya.
LOVENESS NAYE AKAZUNGUMZA
“Mimi Linda alikuwa rafiki yangu, alibadilika tu kwa sababu ya kunionea wivu. Ni uongo mtupu,” alisema Loveness na kuongeza:
“Kiukweli tuligombana kwa vitu tofauti. Alikuwa anaishi kwangu nikamfukuza kutokana na tabia zake lakini nashangaa haya mambo yamekua makubwa hivi sasa.”
SIASA ZATAJWA
Loveness: “Mimi naamini haya maneno ya Linda yamechochewa na siasa. Unajua tangu tufungue tawi la CCM DC, imekuwa tabu sana. Maneno mengi yanazungumzwa. Mfano, mimi na Linda tuligombana karibu miaka saba iliyopita lakini hayakusemwa, nilipofungua tawi la CCM tu ndiyo mambo yakawa makubwa.
“Wakaanzisha mpaka ukurasa wa kikundi Facebook, wakawa wananitukana. Mimi sishangai sana kwa maana Linda ni Chadema damu na mimi ni CCM damu, hizi ni siasa tu.”

No comments: